Waziri Nape kwanini husemi ni vigezo gani ambavyo Starlink hawajatimiza? Au wamegoma sharti la kuzima mtandao muda wowote mkiamua?

China akileta yake kwa kuwa ni mtu wa kitu kidogo kama sisi tu mambo yatakuwa yale yale tu kama ilivyo Tigo, Voda na Halotel. Japo vifaa vitakuwa bei rahisi sio kama vya Elon.
 
Huyu ni mwendawazimu tu kama wengine na kumsikiliza ni kucheza ngoma ya kichaa. Watu ambao wapo kwenye mchakato wa kuifanya star link ije Tanzania hebu endeleeni kuchochea kuni moto uwake.

Ongezeeni kuni kwa wingi ili huyu jamaa afike point ajue kuwa yeye hii taaluma ya mawasiliano hana analolijua hata kidogo. Na wapo watu wenye weledi wao ndio wanatakiwa kushika hapo alipokaa yeye.
 
Ngoja nikuulize swali, hapo uwanja wa ndege tu ukienda kuna mashirika ya ndege watu hawamudu nauli yake au kuna madaraja ya ndege mfabo business ambalo kuna watu hawamudu kulipia, je hiyo ina maanasha kuwa hayo mashirika ta ndege unatakiwa kufungiwa kutoa huduma sababu raia wengi hawamudu gharama?

Kuna hotel kama Ngurdoto, Serena, Kempisk na ile ya chini ya maji iliyopo Zanzibar, watanzania wengi hawamudu gharama ya hizi hotel, so zifungwe kwasababu kuna hotel cheap?

Shule kama IST, Fedha na zinginezo, ni za mamilioni ya pesa kwa mwaka ambayo watanzania kwa asilimia 80% hawana jeuri ya kusomesha watoto zao pale, je zifungwe ili na wale wanaosomesha watoto wao wakose huduma?

Hebu tujifunze kuwa positive na Maisha not always kuwa negative na kupenda kurudisha wengine nyuma kwasababu ya wachache wasiojua maana ya kupiga hatua na hofu ya mabadiliko na maendeleo. Hii Dunia na inchi ni yetu sote ukiwa hauwezi jambo pisha waoweza.
 
ingia katika taarifa zao, hizo kelele hazina maana yoyote... wapo mbioni kuwasha kwa Tanzania tena wapo Q2...

Specific Time Periods: Typically, Q1 refers to January, February, and March;

Q2 refers to April, May, and June;

Q3 refers to July, August, and September;

and Q4 refers to October, November, and December
.

kuna nchi zingine haijulikani ni lini...

umebakia wajibu wa mtoa huduma kutekeleza aliyoambiwa ili apate ruhusa rasmi

akijichelewesha ni yeye mwenyewe sababu utekelezaji umebakia kwake yeye na ndio maana ameiweka Tanzania katika Q2, Uganda Q4
 
Reactions: 511
Wewe hebu tumia akili wewe? Usalama gani huo ambao unazungumzia kama mtoto mdogo anaetuhadhithia story za vijiweni?

Usalama wa inchi mnatumia TikTok, Instagram, WhatsApp, na hizo internet service wangetaka kuwa spy mbona kazi rahisi huyo Elon awaspy kwa lipi taifa la viongozi unproductive kama hili? [emoji848]

Kama unaona Star link ni tatizo basi itakuwa kwako tu usilazimishe huduma ambayo wewe hauihitaji basi ukadhani Tanzania nzima hauihitaji huduma hiyo.

Kwann uwajibie watu, Kenya ilikwama wewe unaishi Kenya au unatutungia story za vijiweni?

Wewe una uhakika gani ilikwama, Kenya nzima wanatumia star link?

Hebu muwe na hoja za msingi mnatia watu hasira hapa.
 
Gharama kuwa kubwa wanajua kwenye star link mbona wakinunua magari ya mamilioni ya pesa kwa kutumia kodi zetu huwa hawazingatii gharama? [emoji848]

Upumbavu tu.
 
Hii ndio point ya msingi mzee. Unajua nachukia sana kuona tunacheza kidali poo kwenye maswala ya msingi. Mtu m'moja tu anakwamisha taifa kupata huduma ya uhakika ya internet kwasababu zake binafsi.
 
Hizo hela wanawekezaje na hizo kampuni ni binafsi, kama wameshindwa biashara ya internet wajikite kwenye biashara ya mawasiliano ya kawaida yaani simu na sms.
 
Embu ❎Hebu✅
 
Hii starlink tunapiga makelele tu hapa, cost za kununua vifaa zipo juu sana
Wewe ndie utakuwa unanunulia watu? Watakaomudu watanunua wewe na hizi akili za umasikini utabakia kutumia hizi bundles zenu za buku buku za kuibiwa unajiunga saa moja kamili, saa moja na dakika tano unaambiwa umetumia 75% ya bando lako.

Upuuzi wa karne huu.
 
Watu mipovu kama ya omo inamwagika hapa,
Wanajifanya watalamu wa hayo mambo, kumbe ni majuha tu hata hawajui ni masharti gani hayajakamilika. Pathetic
 
Sasa tufanyaje tuendelee na haya maisha kwa kuogopa gharama lkn badae litukute tena kama hili lililotokea.?!
hili tukio la mpito, bado nakazia statement ya awali
 
Kuna unlimited airtel, vodacom, tigo pamoja na ttcl fiber zote hizo unlimited zina gharama nafuu kushida starlink, au huzifahamu?
 
👊
... Starlink ikija 'malaika wa mitandao' wa Bongo hana kazi!
😅
NB: 'Malaika wa mitandao' wa Bongo alitufanya visivyo baada ya 'UCHAFUZI' uliopita!
 
Kwa sisi tunaoifahamu hii serikali ya ccm ni lazima hapo wameona kuna kitu kinatishia maslahi yao kisiasa na hao wanaosema oh sijui usalama wa nchi ni walewale chawa wao.

Leo hii kwa teknolojia ilivyokuwa mtu anakufanya vyovyote anavyotaka hata akiwa amelala nyumbani kwake na wewe usiye na tekinolojia yoyote huna cha kumfanya, hivyo swala hapa sio usalama ila ni woga wa ccm kwamba watabanwa kufanya hujuma waliyozoea kufanya. Period.
 
Nchi zimeathirika sawa, vipi watumiaji wa starlink nao waliathirika? Jibu la waziri la kienyeji sana
 
Hii si nzuri, ni personal attack.
 
.Yaan star link, kampuni ya kisasa na yenye technology ya juu kabisa duniani, inaweza kukosa documents muhimu? Kumbe ndio maana huyu wazir alipata four ya mwisho kabisa form four. Yaan anajibu swali muhimu kirahisi hivi? Watanzania tujitafakali sana, tulimkosea nn Mungu mpaka vilaza kama hawa wawe mawazir.
 
Starlink hawana % udalali anaoupata kama apatavyo kwenye mitandao ya huko bongo.

Starlink wanaoperate kwenye standard za kimataifa policcm hawawezi kwenda tu na bunduki zao kudai taarifa za wateja bila utaratibu kama ambavyo Vodacom, Tigo walitoa taarifa za kina Kabendera , Mbowe , Tito Magoti n.k kwa amri tu bila utaratibu wa kimahakama.

Starlink hawatokubali kuzima mtandao ili majizi ya CCM yalivyokata internet siku 5 ili kuiba kura na kujitangazia ushindi feki.

Kivuli anachojificha Nape cha uwepo wa ofisi mbona , Meta, X, Google hawana ofisi Tanzania na wanatoa huduma?

Huyo failure hiyo ofisi imemzidi uwezo ila ndio vile anabebwa bebwa kutoka Msoga anaendelea kuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…