Waziri Nape kwanini husemi ni vigezo gani ambavyo Starlink hawajatimiza? Au wamegoma sharti la kuzima mtandao muda wowote mkiamua?

Waziri Nape kwanini husemi ni vigezo gani ambavyo Starlink hawajatimiza? Au wamegoma sharti la kuzima mtandao muda wowote mkiamua?

Kigezo ni je mtatupa uthibiti kama wakati wa uchaguzi tufunge internet...
Yeye anachotaka ni access control ya data Kwa maslahi ya chama...
Na ndio lengo ya kutaka ofisi hapa ni ili wadeal na Mtu uso Kwa USO hakuna kingine
 
Nape akiona hivi anajisikiaje?

Screenshot_20240515_200424_X.jpg


View: https://twitter.com/usembassytz/status/1790060919126392920?t=1wAAvcoljgWyGg27H7A0Iw&s=19

Alafu CCM wamemkalia kimya, hawajui hii ni fimbo itakayotumiwa na wapiga kura wengi kwenye chaguzi zijazo
 
Kigezo ni je mtatupa uthibiti kama wakati wa uchaguzi tufunge internet...
Yeye anachotaka ni access control ya data Kwa maslahi ya chama...
Na ndio lengo ya kutaka ofisi hapa ni ili wadeal na Mtu uso Kwa USO hakuna kingine
Ger.PNG

hapo juu Ujerumani anamakubaliano yake ya ziada kulingana na sheria zao... unaweza ipitia hiyp sheria inataka nini... na sisi tukiwa na matakwa yetu ni sisi... hawa na taka mpaka mteja apewe taarifa za uhakika wa speed ya matumizi ili ikishuka kulikokawaida ajieleze...

UK na nchi nyingi za Ulaya hii ndio aina ya makubaliano yao
uk.PNG

ukk.PNG




Zambia, Kenya na nchi nyingi za Afrika hii ndio aina ya makubaliano yao

zambia.PNG



Tuendelee kuiamini serikali yetu... serikali za afrika hazina mpango na maswala ya mazingira, wenzetu ulaya huko nk wanazingatia vingi kwenye mikataba yao mpaka maswala ya mazingira


 
Nape akiona hivi anajisikiaje?

View attachment 2990950

View: https://twitter.com/usembassytz/status/1790060919126392920?t=1wAAvcoljgWyGg27H7A0Iw&s=19

Alafu CCM wamemkalia kimya, hawajui hii ni fimbo itakayotumiwa na wapiga kura wengi kwenye chaguzi zijazo

 
Akiwa anahojiwa kutoka katika televisheni ya Wasafi (Wasafi TV) Waziri Nape amesema kuwa serikali haina matatizo na Starlink, kinachofanya washindwe kutoa huduma zao nchini ni sababu hawajakamilisha masharti, na kama wakikamilisha basi wataruhusiwa kutoa huduma nchini.

Msikilize hapa


====
"Nimezungumza hapa, kama nchi tunamchakato wa kuwa na Satelite ambao tutaukamilisha mapema tu, iwe ni alternative yah hizi cable. The best ni cables lakini satellite ni njia mojawapo, na Starlink ni kama watoa huduma wengine ambao wanaleta huduma za mawasiliano walikuja wakaomba leseni.

"Sasa mfumo wetu wa lesseni unaoingia kwenye mtandao kidijitali unajaza taarifa mbalimbali, sasa baadhi ya nyaraka walikuwa hawana, kwahiyo walipoenda wakafika mahali wakagota na nyaraka zile hawana, sisi tuliwaambia kamilisheni. Wakikamilisha maombi yao na yakaletwa mezani kwangu siku hiyo hiyo nasaini, hatuna matatizo nao.

"Nasikia watu wanasema wamezuiwa, hatujazuia mtu. Tumewaambia kamilisheni utaratibu. Hatuwezi kubadilisha taratibu tulizoziweka ambazo watoa huduma wote wamezifuata kwasababu ya mtu mmoja ambaye hana cheti chake cha form four sijui cha wapi. Fuateni utaratibu tu na kila kitu kipo mtandaoni wala hauitaji kwenda kusoma. Kwahiyo wakikamilisha watakuja.

"Lakini hata baadhi ya nchi ambazo wanapata huduma hiyo ya Starlink na wenzake ni katika nchi zilizoathirika. Kwahiyo kwenda kudanganyana kwamba eti ndio suluhu la mwisho kabisa, tunadanganyana. Mimi najua katika nchi 11 karibia nchi 2..3 zinapata huduma na zimeathirika."
====

Ni masharti gani hayo yanayosemwa kila mara kuwa Starlink hawajatimiza? Yaani Nape anataka kutuamisha kabisa kuwa Starlink wamekosa cheti cha kutoa hudumu nchini?

Wameweza kukamilisha documents kwa nchi nyingine halafu ndio washindwe kukamilisha kutoa documents Tanzania, nchi ndogo ambayo inajikongoja kwenye karibu kila kitu?

Nape tuambie ukweli, acha kuzunguka zunguka, ukiangalia uchaguzi mkuu upo puani na historia imetufundisha vyema vile mnatufanyia wananchi linapokuja suala la mtando.

Kwa ninavyoona Serikali itakuwa imetoa sharti kwa Starlink na Elon Musk kuzima mtandao kila serikali itakapotoa agizo hilo, na kwakuwa Elon ni champion wa uhuru wa kujieleza akawatolewa nje basi na nyie serikali mkashupaza shingo.

Inaonesha mwakani ngoma nzito kiasi kwamba mko tayari hata kuacha taifa liingie hasara ya mabilioni ya pesa sababu ya kukosekana kwa internet ili tu mjihakikishie kuendelea kubaki madarakani.

Wakuu, maonaje kuhusu hili? Sababu hii ina mashiko? Kama haina mashiko unafikiri ni sababu gani au document gani ambayo Sterlink wameshindwa kutimiza ili wapewe leseni ya kuhuduma ya mtandao nchini?
🤣
 
Starlink ni ghali.

Huko Kenya gharama za kununua vifaa ni sawa na Tsh1.7m

Kifururushi cha chini kabisa Tsh130k/mwezi

Ipo Kenya karibia mwaka ila wanaotumia hawafiki 3000. Sasa utatobokaje mfuko wakati providers wengine kama zuku wanakupa huduma kwa bei che?

Mimi naona Nape atakua anashirikiana na kina voda ambao hawataki kupoteza wateja wao wakubwa, starlink itawaiba hao maskini hawatoimudu
Hoja yako dhaifu sana mkuu, huduma iruhusiwe na watakaomudu wajiunge, kwani ina madhara gani wakiwepo. Wangapi wanamudu kununua hizo simu za kuanzia USD 2000? mbona hazijazuiliwa kwa sababu wengi hawazimudu?
 
Back
Top Bottom