Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Nape Nauye amepata mashambulizi makubwa sana mengi yakiwa yanatokana na historia yake kisiasa. Yapo makosa ya kisiasa ameyafanya na sasa yanamgarimu sana.
1. Kutumia goli la mkono kushinda uchaguzi
2. Kulazimisha tume ya uchaguzi imtangaze mshindi bila kupingwa
3. Kumtukana JPM akiwa hai
4. Kwenda ikulu kuomba msamaha akimulikwa na camera
5. Kumkejeli JPM baada ya kusikia amefariki
6. Kutukana wanasiasa wenzake ili apate umaarufu
7. Kumtukana Tundu Lisu
8. Kuwa na elimu inayotiliwa mashaka.
Haya na mengine yamemfanya ashambuliwe kirahisi na wapinzani ndani na nje ya chama bila kupata misaada.
Ukitaka kupima chuki waliyonayo wananchi dhidi yake, hana mtetezi kwenye vyombo vya habari anavyoviongoza pamoja na mitandao ya kijamii. Kila anapotamkwa vibaya watu wanashangilia.
Japo baya zaidi, ni mtu anayeamini kwenye kukamata, kutesa na kutweza utu mara tu anapopewa madaraka. Siyo mtu wakushirikiana na jamii bali always anawaza kunufaika kisiasa bila kujali wanaathirika wangapi.
Nimemsikiliza alivyohojiwa BBC kuhusu issue ya Makamu wa Rais, kwa namna alivyojibu kwa jazba na bila kujikita kwenye hoja ni wazi kwamba angekuwa na uwezo waliofungia BBC angaifungia. Waziri kutamka kwamba chombo cha habari kinashabikia mambo ya ovyo kisa wameuliza jambo ambalo ni kinyume na mtizamo wake ni tafsiri ya kiburi cha madaraka.
Kama Taifa naamini hiii interview imetuchafua sana kimataifa......imeonyesha wazi kwamba siyo kwamba vyombo vya ndani vinashindwa kuhoji bali VIKIHOJI WAZIRI ANAWEZA HATA KUELEKEZA ANAYEHOJI AFUNGWE AU AKAMATWE.
Watoto wa viongozi punguzeni ulevi wa madaraka, wazazi wenu wasingekuwa viongozi leo msingeongoza hata kitongoji coz mnakosa qualities.