Waziri Nape Nnauye tusaidie kutumbua huyu mama na Bodi yake.

Waziri Nape Nnauye tusaidie kutumbua huyu mama na Bodi yake.

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Joyce%20Fissoo2.jpg


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fisso akiongea na eNewz ya EATV amesema hana taarifa na wala hajui kama kuna wizi wa kazi za wasanii katika nchi hii.

Kumekuwa na kilio kikubwa kwa muda mrefu juu ya wizi wa kazi za wasanii wa muziki na filamu kutoka kwa wasanii wenyewe na wameshapeleka malalamiko yao mara kibao kwenye ofisi yake, kitendo cha mtendaji wa bodi hio kuibuka kwenye media kusema hajui kama kuna wizi huo ni dhahiri kuwa kwenye nafasi hiyo anapwaya, au ana maslahi binafsi na wizi huo au bodi haijui inafanya nini.

Kumekuwa habari za kuaminika kuwa kuna kundi la Wahindi kama 15 hivi maeneo ya Kariakoo, Mnazi Mmoja na Upanga wanamiliki vifaa vya kurudufisha kazi za wasanii wetu hapa nchini kwa maelfu mara tu zinapotoka, na kuna ushahidi wa wazi kuwa wanashirikiana na baadhi ya watendaji wa serikali na wa bodi hii.

Najua una uwezo mkubwa wa kufuatilia hili kwa kina na kubaini ukweli wake, anza na huyu mama na bodi yake utabaini madudu mengi sana.

Wasanii wa nchi hii wamekuwa migongo ya watu wengine kupanda kula matunda ambayo hawajawahi hata kuyatolea jasho, huku wao wakibaki kuwa watu wa kuimba kwenye party za birthday za watu maarufu.
 
Inabidi ajifanye hajui, maana hata akisema anajua hana ubavu wa kuwakamata maana unaweza ukakuta hata huyo Nape anakula chake
 
wasanii inabidi wapambane na wasambazaji maana wao hawasambazi kazi zao wanawauzia wahind mengine hayawahusu sasa hicho kilio cha kuibiwa sijui ayewaibia ni step au kuuzwa barabarani ndo kesi
 
Back
Top Bottom