Waziri Ndaki na Katibu (Mifugo) Nzunda, Uhalisia kuhusu kuomba kusitisha mafunzo atimizi (internship) kwa Madaktari wa Mifugo

Halafu nani aliwaambia wajiite madokta?
Acha dharau wewe..hao jamaa wanavyo visoma na md yako huwapati hata robo.

Wewe unasoma kiumbe hai mmoja wao wanasoma karibia mamalia wote.

Kwahiyo kama udokata hawa ndio walistahili kabisa hilo jina.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini bado upo SUA, cheki na mwenyekiti wa TVA Prof. Karimuribo, mjuze hilo.
 
Kwa hiyo intern serikali iseme, kijana ajitolee!
Siyo apangiwe eneo la kwenda!
Kila mtu afanye intern nyumbani kwao ofisi za kata au vijiji!

Wasiwapangie mfano, mtu katokea Ukerewe akawe intern Newala!
Pole Dr Ila vets wanapiga Sana hela!

Kila house call! Nilipo tumezunguka ni wafugaji mbwa, Ng'ombe, mbuzi Katoliki, kuku kienyeji, layers, broilers, chotara. Na Dr anayetumika ni mmoja. Wengine wana maduka ya pembejeo n.k
 
Bora wafanye hivi kidogo tutasaidika.

Ila sasa internship yenyewe wameweka vipengele vingi ambavyo vinatubana sana sisi tusio kua na ramani yoyote ( jobless) kutumia pesa nyingi ambazo hatuna.

Ni vyema wapitie upya kanuni za intern, maana tunaoteseka ni sisi masikini.
 
Kuna watu ambao wako kwenye dhamana wanafanya maamuzi ya hovyo sana kisa wao walishavuka kwenye hatua hiyo, huwezi kutunga sheria ya kuwataka vijana kwenda internship bila kuweka utaratibu wa wao kulipwa posho kama wenzao kwenye wizara ya afya........huu ni uzwazwa na hakuna mtu aliyewashikia kisu kuleta hiyo sheria kwa pupa, hovyo sana......
 
nakumbukaga sana Ile kauli kwamba ipo siku vizazi vijavyo vitakuja kuchapa bakora makaburi yetu Kwa mambo ambayo wazee wetu waliopewa nafasi huko kwenye mfumo wanayoyafanya......

Sometimes unawaza labda mtungaji Sheria kasomea mazingira mazuri that's y anaona kama n simple Tu kujitolea .........
 
Ila kwenda internship mwaka mzima bila malipo sio mchezo, Sijui wanaofanya haya maamuzi wanafikiria nni!!!!!!!????
 
Kweli ndugu, yaani wanatunga sheria bila kujui jinsi gani zitatekelezwa. Au bila kua na mipango ya utekelezaji wa hizi sheria
 
Wale ni ma-Afisa mifugo na siyo madokta
Hata mkituita wakulima ni sawa tu, nyie kwenye Wizara yenu si mna watu wakuwatetea.

Sisi wenzetu Veterinarian tulio wapa vyeo ndio wanatukandamiza. Kwaio sioni ajabu kutuita jina lolote. Maana hatuna wa kututetea.
 
P

Vet Surgeon, ni lazima uelewe kuwa matatizo yako yatatuliwa na wewe mwenyewe kwa kiasi kikubwa. Nachoweza kuwashauri ni yafuatayo:
1. Fikisheni malalamiko yenu kwa viongozi wenu wa TVSA.
2. Mji'organise wote mfanye utaratibu wa kutuma wawakilishi kwenda Wizara yenye dhamana ya mifugo ili mfikishe malalamiko yenu.
 
Watatuaje matatizo wenyewe?

Vet surgeon alisema yote hayo wameshafanya ila wizara husika na viongozi wa TVSA ndio tatizo
 
Tena kaburi la huyo kichomi waliyempeleka hapo; Anajiita Dr ( kama Presidenti wa mawe, miti na vichuguu) Tixon Nzunda ! Shughuli wanayo , huwa anaongozwa na bichwa lake lenye piihechidii....... simalizii asije kuni beni saa8 maana ndio anachojua tu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…