Wizara ya Ardhi
Member
- May 14, 2024
- 94
- 75
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amemuelekeza Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Ruvuma kuifuta Hati ya Ardhi kwa Bw. Steven Mapunda ambaye alikabidhiwa bila kufuata utaratibu katika Kijiji cha Mwanamango Manispaa ya Songea.
Mhe. Ndejembi ametoa agizo hilo Septemba 22, 2024 baada ya kufika katika kijiji hicho kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.
Mgogoro huo unamuhusisha Bw. Mapunda aliyemilikishwa ekari 45 za mashamba ya wananchi wa Mwanamango bila kuwalipa fidia kama sheria inavyoelekeza.
“Ninamuelekeza Kamishna wa Ardhi wa Mkoa kufuta hati ya Bw. Mapunda kwa sababu wananchi hawakushirikishwa na wala hawakulipwa fidia. Kwa hiyo maamuzi yangu leo ni kwamba hiyo hati iondolewe papimwe tena na wananchi wamilikishwe maeneo yao kwa mujibu wa sheria.
Soma Pia: Waziri Ndejembi Ataka Watendaji Ardhi Kuondoa Urasimu na Kutoa Hati kwa Wakati
"Na hapa ninafahamu ni wananchi takribani 30 ambao maeneo yao yalipimwa bila ridhaa yao na bila fidia. Hivyo ninaelekeza wamilikishwe maeneo yao,” amesema Mhe. Ndejembi.