Waziri Ndejembi aagiza Watumishi saba ardhi kuchukuliwa hatua za kinidhamu

Waziri Ndejembi aagiza Watumishi saba ardhi kuchukuliwa hatua za kinidhamu

Joined
May 14, 2024
Posts
94
Reaction score
75
Dar es Salaam

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi saba wa wizara hiyo Mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma za makosa waliyofanya kwenye sekta ya Ardhi.

Mhe. Ndejembi ametoa kauli hiyo mkoani Dar es Salaam wakati alipokutana na watumishi hao ambao wamekiri kuhusika na baadhi ya migogoro ya ardhi katika Mkoa huo ambapo kupitia kikao hicho Waziri wa Ardhi amemwelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuihusisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kushughulikia suala hilo.

"Namuelekeza Katibu Mkuu kuwahusisha wenzetu wa TAKUKURU kupitia majalada yote ya watumishi hawa, Katibu Mkuu wachukulie hatua kali za kinidhamu ili tuweze kuondokana na changamoto ya wananchi kutopata huduma bora kwenye sekta ya ardhi,” amesema Mhe. Ndejembi.

Baadhi ya changamoto katika sekta ya ardhi mkoa wa Dar es Salaam zibebainika baada ya watumishi wanaotuhumiwa kukiri kuhusika moja kwa moja na tuhuma zinazowakabili kufuatia kupitiwa kwa majalada ambayo watumishi hao walikua waliyafanyia kazi.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Lucy Kabyemera pamoja na watendaji wengine wa wizara.

-----‐-----mwisho--------
 
Tuhuma gani hasa specifically?

Wizara ya Ardhi pia mnapaswa kuwatupia jicho Kali zaidi Wenyeviti (Mahakimu) wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya yaliyopo hapa nchini. Wengi wao Kama siyo wote Wana matatizo makubwa Sana ambayo kamwe hayavumiliki, Wananchi wengi Sana wamekuwa wakiumizwa na Watu hao (I e. Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi), Wahalifu wa Ardhi, Matapeli na Waporaji wa Ardhi wa Wameunda "Syndicate" au Cartel yao na hao Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi ili kuwadhulumu Ardhi zao Wananchi Wanyonge, na Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya yamekuwa yakibariki officially uhalifu unaofanywa na hao Matapeli au Majambazi ya Ardhi.

USHAURI WANGU KWA WIZARA YA ARDHI ILI KUDHIBITI UHALIFU KWENYE MASUALA YA ARDHI HAPA TANZANIA:-
1. Chini ya Wizara hii, anzisheni Kitengo Maalumu cha Kuzuia, Kudhibiti na Kushughulikia suala hili la Migogoro ya Ardhi au Uhalifu wa Ardhi hapa nchini.

(I) Chini ya Kitengo hiki, anzisheni Dawati Maalumu la Wananchi kuweza Kuwasilisha taarifa za Siri ili kufichua Uhalifu au Utapeli kwenye Ardhi. Wananchi waruhusiwe kuwasilisha kwa Siri taarifa za Namba hii 'Whistle blowing' ili kufichua Majina yote ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya uhalifu kwenye masuala ya Ardhi sambamba na uhalifu wao waliohusika nao.

Baadaye Wizara ya Ardhi unaweza kujiridhisha na usahihi au Ukweli wa taarifa hizo kwa kufanya Uchunguzi wake wa kimya kimya dhidi ya Mtumishi wa Ardhi aliyetuhumiwa.

(ii) Kwenye Ofisi zote za Ardhi wekeni Matangazo ya kuwataarifu wananchi juu ya Utendaji wa kiuhalifu watakaobaini dhidi ya Watumishi wa Ardhi.

2. Utaratibu wa Uendeshaji wa Mashauri ya Ardhi kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ubadilishwe haraka sana, Wenyeviti (Mahakimu) wa Mabaraza ya Ardhi;ya Wilaya wamekuwa wakihujumu Sana Mafaili ya Kesi za Ardhi kwa Kubadilisha Maelezo ya Mashitaka au Mwenendo wa Kesi za Wadaawa.

Wenyeviti (Mahakimu) wa Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya watakaobainika kuwa wamejihusisha na Uhalifu wa Kuhujumu Mafaili ya Kesi za Ardhi wanapaswa wafukuzwe kazi mara Moja bila kuchelewa.

Mahakimu hao pia walazimishwe kuwapatia Nyaraka za Mwenendo wa Kesi Wadaawa katika Kesi za Ardhi ili wazitoe photocopy kwa ajili ya kutunza Ushahidi wa Mwenendo wa Kesi. Hii itawadhibiti Mahakimu hao wasiweze kubadilisha Maelezo ya Kesi yaliyopo kwenye Mafaili ya Kesi za Ardhi. Nyaraka za Photocopies za Mienendo ya Kesi zinazotolewa kwa Wadaawa kila siku baada ya usikilizaji wa Kesi husika zinapaswa kugongwa Mhuri wa Mahakama na Hakimu husika anapaswa asaini na kuthibitisha kwamba ni "Certified True Copy of the Original Proceedings."

TANBIHI:
Wizara ya Ardhi inapaswa itambue kwamba Haki za Watu kwenye Ardhi zinadhulumiwa Sana na hao Wenyeviti (Mahakimu) wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya.

Ninayo mifano ya Kesi nyingi Sana kuhusiana na suala hili, Watu wengine tayari wamefariki dunia kutokana na mshituko wa moyo kwa hujuma za namna hii.
 
Kule Tegeta wamesababisha migogoro mingi kwa kupora viwanja vya watu na kuwauzia watu wengine,Mmoja wa wahusika anaitwa Gaudence.
 
Back
Top Bottom