Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma, Mhe. Deogratius Ndejembi amejiandikisha kwenye Daftari la Mpiga Kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika kitongoji cha Mpela Wilaya Chamwino, Dodoma leo.
Zoezi hilo limeanza leo nchi nzima na kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan na litaendelea hadi Oktoba 20, 2024.