Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Ndugu Faustine Ndugulile hapo zaidi ya miezi minne ulikuwa unashughulikia kero zinazo wakabili watanzania hasa juu ya wizi wa vifurushi vya simu. Maana watu wengi walikuwa wakilalamika kuwa wakinunua vifurushi hata kama hawajatumia sana vilikuwa vinateketea kama karatasi inachomwa moto.
Ulipoteuliwa tu kuwa waziri wa Tehama ukasema utaondoa hii kero. Na kwa kuahidi watanzania kuwa utatengeza kanuni ambazo zitakata mzizi wa fitina na gharama za vifurushi zitapungua. Mfano ulidai kuwa bei ya mb moja itakuwa kati ya sh1-9.
Tarehe mbili ya mwezi huu kanuni zako mpya zilianza kutumika. Lakini mambo yakawa mabaya zaidi kiasi cha kuzua kilio cha umma. Umeamua kunyoosha mikono juu.
Swali kubwa la msingi kama hapo awali watanzania walikuwa wanaibiwa, mbona unarudisha tena waibiwe?