Waziri Ndumbaro acha kupotosha umma, Tunataka Katiba Mpya iwe na uwezo wa kutatua changamoto zetu. Ikiwezekana kumshtaki Rais na Mawaziri

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Huko Usa haki zikivunjwa unaenda mahakamani na mahakama ipo hutu
Screenshot_20230423-173813.jpg
 
Waziri kaelezea kwa mapana zaidi kwa kifupi sana lakini alichomaanisha waziri ni kwamba katiba mpya haitabadili watu wabaya kuwa wema kwa maana rahisi ni kwamba mtu mbaya ataendelea kufanya ubaya kwa dhamira na nia sio kwa sababu ya katiba mpya.
 
Wenye mawazo kama haya ni wajinga.binadamu anaongozwa kwa taratibu sio utashi au matakwa yake mwenyewe.kuwe na katiba nzuri kuwe na sheria nzuri kuwe na taasisi na mifumo imara ya kuendesha nchi alafu tuone huyo atakayechezea nchi.tukisema nchi iendeshwe kwa dhimira njema za mtu atakavyojisikia hiyo itakua ni nchi ya ovyo kwasababu waliopo ndo hawa hawa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Waziri kaelezea kwa mapana zaidi kwa kifupi sana lakini alichomaanisha waziri ni kwamba katiba mpya haitabadili watu wabaya kuwa wema kwa maana rahisi ni kwamba mtu mbaya ataendelea kufanya ubaya kwa dhamira na nia sio kwa sababu ya katiba mpya.
Hatutaki katiba ya kubadili watu kuwa malaika, bali katiba yenye meno, sio hii katiba inayofuatwa kwa utashi wa rais aliyeko madarakani.
 
Tangu katiba ya 1977 kuna mabadiliko mangapi yamefanywa ? Ni zaidi ya mabadiliko makubwa 13 hivyo katiba inabadilika kulingana na mahitaji ya wakati, kulingana na sera za nchi na hata matamanio ya watawala au Wananchi. Hata itakayoitwa katiba mpya ikiwepo Kuna siku atapatikana kiongozi wa kuibadilisha na mambo yakawa ni Yale yale ya kudai katiba mpya.

Cha msingi tuanze kubadili watu kwanza, tuwajengee wa kuishi kwenye maadili
 
Hii katiba ya 77 inatoa mamlaka ya uungu kwa rais, ndio maana mabadiliko yake yanategemea hisani ya rais, lakini tukiwa na katiba iliyo juu ya rais na kulindwa na mifumo sio rahisi kutokea kiongozi akaichezea. Unapotaka Kupata katiba mpya, kisha wale wasioitaka ndio wakawa vinara wa kutaka kuiandika ni wazi tutabaki kila siku tunadai katiba.

Ili tuweze kupata katiba ya kweli ya wananchi, ni aidha yatokee machafuko, au mapinduzi ya kijeshi, hapo tutapata katiba ya kweli ya wananchi.
 
Acha upuuzi. Hii katiba ya sasa inaruhusu raia kumshitaki rais au mbunge akifanya ufisadi?
 
Umeandika takataka, nenda Kenya, Wana katiba mpya, bado wanabishana bei ya unga, narudia bei ya unga, sio barabara za rami
Puuzi kubwa huna akili. Unatumia makalio kuwaza. Bila katiba madhubuti hayo maandamnao yangefanyika.? Tunataka muwajibishwe
 
Acha upuuzi. Hii katiba ya sasa inaruhusu raia kumshitaki rais au mbunge akifanya ufisadi?
Kwa hiyo mabadiliko ya Katiba mpya yanayopiganiwa na CHADEMA lengo ni Rais ashtakiwe ? Basi tuna safari ndefu sana na wengi wanaolilia katiba mpya hawajui lolote ila ni mkumbo tu.
 
Umeandika takataka, nenda Kenya, Wana katiba mpya, bado wanabishana bei ya unga, narudia bei ya unga, sio barabara za rami

Katiba inahusika na mambo ya utawala, na wala sio chakula. Usichanganye katiba na tumbo.
 
Kwa hiyo mabadiliko ya Katiba mpya yanayopiganiwa na CHADEMA lengo ni Rais ashtakiwe ? Basi tuna safari ndefu sana na wengi wanaolilia katiba mpya hawajui lolote ila ni mkumbo tu.

Rais kutokishitakiwa ni sehemu inayofanya katiba ya sasa kutokufuatwa kwa usahihi. Hilo la kushitakiwa kwa rais ni sehemu tu ya katiba inayotakiwa. Usilete upotoshaji wa kijinga tafadhali.
 
Hii katiba ya 77 inatoa mamlaka ya uungu kwa rais, ndio maana mabadiliko yake yanategemea hisani ya rais, lakini tukiwa na katiba iliyo juu ya rais na kulindwa na mifumo sio rahisi kutokea kiongozi akaichezea. Unapotaka Kupata katiba mpya, kisha wale wasioitaka ndio wakawa vinara wa kutaka kuiandika ni wazi tutabaki kila siku tunadai katiba.

Ili tuweze kupata katiba ya kweli ya wananchi, ni aidha yatokee machafuko, au mapinduzi ya kijeshi, hapo tutapata katiba ya kweli ya wananchi.
Tuacheni kupotosha kwamba katiba ya JMT ni Rais na Rais ndiye Katiba na tukibadili mtazamo huu basi hatutalaumu.

Hata Kama katiba itashtaki Rais kama mnavyotaka ni lazima mtambue itampa nafasi ya kujitetea na hapo lazima atashinda, kwa nini? Rais ni taasisi na anatenda kwa kadiri ya mahitaji ya Taasisi kwa maana anapokea na kupewa ushauri. Tafsiri yake kosa la Rais ni kosa la kitaasisi zaidi, sasa unafikir kweli ni Rais kumshinda ukimshtaki?
 
Sina shaka na ninaposema kuwa katiba yetu ni rais, na kibaya zaidi imetoa nafasi ya yeye kuamua anavyoona. Hujui kuwa rais halazimiki kufuata ushauri wowote?

Hilo kuwa urais ni taasisi ipo kimadharia zaidi, ndio maana unaona hata sheria zetu nyingi zinatungwa kuendana na rais aliyeko madarakani. Udhaifu wa mifumo yetu umechangiwa sana na madaraka ya kimungu aliyo nayo rais. Ndio maana unaona amri kutoka juu ambayo ni mamlaka ya urais, ina nguvu kuliko hata katiba na sheria. Siku rais atapinguziwa madaraka haya ya kimungu, ikiwemo na kushitakiwa, tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwenye eneo la utawala wetu, na mifumo itakuwa na nguvu.

Kwa katiba hii ambayo mahakama zinapewa amri na mamlaka ya urais, ni wazi ukimshtaki rais atatengeneza hukumu aitakayo.
 
Ni kweli tunahitaji katiba mpya lakini watawala watakua tayali kuifuata inavyosema? Tena inabidi Raisi na viongozi wote washitakiwe wakiwa kwenye madaraka au wakiwa wametoka madarakani
 
Back
Top Bottom