Waziri Ndumbaro acha kupotosha umma, Tunataka Katiba Mpya iwe na uwezo wa kutatua changamoto zetu. Ikiwezekana kumshtaki Rais na Mawaziri

Waziri Ndumbaro acha kupotosha umma, Tunataka Katiba Mpya iwe na uwezo wa kutatua changamoto zetu. Ikiwezekana kumshtaki Rais na Mawaziri

Umeandika takataka, nenda Kenya, Wana katiba mpya, bado wanabishana bei ya unga, narudia bei ya unga, sio barabara za rami
Siyo hilo tu. Katiba ya Kenya inasema uteuzi wa Makatibu Wakuu ( CAS), lazima uidhinishwe na bunge. Lakini mwezi March Rutto aliteua na kuapisha Makatibu Wakuu bila idhini ya Bunge
 
Huko Usa haki zikivunjwa unaenda mahakamani na mahakama ipo hutuView attachment 2597231
wakumpotezea usibebe kila kitu toka kwake kashiba huyo hamjuwi mwenye njaa,juzi nilimsikia akisema lilifanyika kosa kuvunga mfumo wa mabalozi kuwa na nguvu kiserikali mana walikuwa wanawajuwa watu wao!!.Kwani kazi ya serikali nini kupitia sensa na serikali ya mtaa hadi alete uzembe wake hapa?
 
Siyo hilo tu. Katiba ya Kenya inasema uteuzi wa Makatibu Wakuu ( CAS), lazima uidhinishwe na bunge. Lakini mwezi March Rutto aliteua na kuapisha Makatibu Wakuu bila idhini ya Bunge
Acha uongo wewe mbumbumbu. Hicho kitu hakiwezekani Kenya ungesikia kesi mahakamani
 
Marekani Trump kapelekwa mahakamani hana makosa mpaka ashikwe na kosa. Hii kutokana na katiba ya marekani sasa hapa kwetu mtu anasema hela ya madafu tena kwenye Dar stock market kainvest mpunga mrefu tu. Lakini hakuna wa kumpelekea mahakamani kwasababu katiba ina mlinda(chama kina nguvu kuliko katiba)
 
Waziri kaelezea kwa mapana zaidi kwa kifupi sana lakini alichomaanisha waziri ni kwamba katiba mpya haitabadili watu wabaya kuwa wema kwa maana rahisi ni kwamba mtu mbaya ataendelea kufanya ubaya kwa dhamira na nia sio kwa sababu ya katiba mpya.
Acha kuwa na mawazo potofu na ya kishetani.
Hao watu wabaya kwa Sasa hawafanywi lolote.Wanaendeleza ubaya. Tunataka katiba mpya na Sheria zake ziseme Mayala akipewa nafasi siyo ya kulambamo Bali ni utumishi na akafanye hivi au vile,ikitokea kafanya hivi au vile katiba na Sheria zake ziseme Mayala afanywe nini
 
Huko Usa haki zikivunjwa unaenda mahakamani na mahakama ipo hutuView attachment 2597231

Mimi ninachoshauri wakati wa kujadili katiba tusifanye kana kwamba tunatoa adhabu au kulipiza kisasi kwa kikundi fulani cha wenye mamlaka. Tuwe na mtazamo chanya kuelekea mabadiriko. Tuongozwe na kupenda kuweka katiba yenye tija kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Tusiongozwe na jazba katika hili. Tuwe watulivu. Maana katiba ina mustakabali wa muda mrefu wa taifa.
 
Waziri kaelezea kwa mapana zaidi kwa kifupi sana lakini alichomaanisha waziri ni kwamba katiba mpya haitabadili watu wabaya kuwa wema kwa maana rahisi ni kwamba mtu mbaya ataendelea kufanya ubaya kwa dhamira na nia sio kwa sababu ya katiba mpya.
Hiyo ni katiba butu, Huyu Jamaa hajui kitu kuhusu katiba iliyojitosheleza. Inang`ata. Hata yeye asingepata hiyo nafasi. Ana uwezo mdogo sana
 
Back
Top Bottom