Waziri Ndumbaro ateta na waandaji wa sherehe za ufunguzi AFL

Waziri Ndumbaro ateta na waandaji wa sherehe za ufunguzi AFL

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Black Engineering kutoka nchini Italia Massimo Fogliati ambao ndio walioandaa sherehe za Ufunguzi wa African Football League Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamefanyika Oktoba 21, 2023 Jijini Dar es Salaam ambapo Mhe. Waziri amewashukuru kwa kufanikisha ufunguzi huo, pamoja na kutoa ajira na fursa kwa watanzania ambao walihusika katika Ufunguzi huo.

Mhe. Ndumbaro amewakaribisha wawekezaji hao kufungua tawi hapa nchini kwakua tayari wana matawi Saud Arabia na Dubai.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji huyo, Bw. Massimo amepokea pongezi hizo na kushukuru Serikali na Wadau wote wa michezo kwa ushirikiano, ambapo ameahidi kurudi nchini kwa ajili ya kutafuta fursa zaidi na uwekezaji.
IMG-20231021-WA0052.jpg
IMG-20231021-WA0053.jpg
IMG-20231021-WA0051.jpg
IMG-20231021-WA0050.jpg
IMG-20231021-WA0049.jpg
 
Huku ndiko kuchangamkia fursa sijui na sisi tunaweza kupata walau kujifunza kidogo
 
Wakati jamaa wakifanikisha ng'ambo ya jirani walikuwa wanaomba liharibike,kifupi muulize ali choki na farasi wake!
 
Kila la kheri wamekunja maokoto yao....makampuni yetu Tz tumejifunza kitu?
 
Back
Top Bottom