#COVID19 Waziri Ndumbaro azindua Utafiti wa kuongeza Utalii wa ndani Tanzania kipindi cha COVID-19

#COVID19 Waziri Ndumbaro azindua Utafiti wa kuongeza Utalii wa ndani Tanzania kipindi cha COVID-19

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Huria, leo tarehe 15 Januari 2022 Jijini Dar Es Salaam, imefanya Uzinduzi wa Utafiti wa Utalii wa ndani na Mchango wa Sekta ya Utalii katika Uchumi wa Nchi kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya Uviko-19.

Madhumuni ya Utafiti huu ni kutaka kujua nini kifanyike ili kuongeza Utalii wa ndani. Pia ni kutaka kujua kwanini idadi ya Watalii wa ndani ya Nchi ni Wachache na nini kifanyike ili Waongezeke?.

Akizindua Mpango huu, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro, amesema Utafiti huu utatusaidia kuongeza utalii wa ndani. "Tunazindua mpango Muhimu sana. Mpango tunaouzindua una Mambo makubwa mawili, Jambo la kwanza ni utafiti kuhusiana na utalii wa ndani, na jambo la pili ni utafiti kuhusiana na Sekta ya Utalii katika Uchumi wa Nchi. Utafiti wa Utalii wa ndani, haujawahi keep fanyika Toka tumepata uhuru. Tulikuwa tunajali sana Utalii wa nje lakini COVID-19 imetupa darasa". Amesema Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Damas Ndumbaro.

Wizara ya Utalii imepata Bil 90.2 kwa miradi yake yote kutoka kwenye mkopo wa tril 1.3 Mkopo wa pesa za COVID-19. Hii pesa itasaidia kukuza uhifadhi na kueneeleza Utalii.

Taasisi nyingine zitakaoshiriki kwenye Utafiti huu ni NBS na BoT. Utafiti utafanywa na Watanzania. Watu zaidi ya 700 wanaenda kushiriki kazi hii.

Utafiti utatupatia takwimu,sababu na njia. Utafiti huu Utashirikisha kaya 33800 Nchi nzima. Waziri amesema Utafiti huu utaongeza Utalii wa ndani na fursa zake.
 
Shida ya utalii wa ndani ni uchumi wa wananchi. Utafiti na sababu za kutafutiza ni siasa na upigaji tu.
 
Back
Top Bottom