Waziri Ndumbaro punguza siasa katika usalama wa wananchi dhidi ya tembo wavamizi

Waziri Ndumbaro punguza siasa katika usalama wa wananchi dhidi ya tembo wavamizi

Kajeba

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2020
Posts
1,057
Reaction score
2,364
Wakuu,

Kwa sasa hali ya usalama wa wananchi wanaoishi maeneo ya jirani na hifahibza wanyama pori umekuwa wa kusuasua kutokana na uvamizi wa tembo katika makazi na mashamba ya watu, pia hata wengine kuuawa

Sasa waziri Ndumbaro amekosa suluhu dhidi ya tembo hao kunusuru usalama wa raia na mali zao zaidi ya kuleta siasa kwamba tembo wamepungua kutoka laki 1 mpaka elfu 60 na kipindi hiko kulikuwa hakuna shida hizi

Kiuhalisia hizi ni siasa dhidi ya usalama wa watanzania, Ndumbalo toa suluhisho kwa sasa wananchi hawahitaji porojo kwani tukianza ujangili na uvunaji wa tembo hao mtakuja kulia ninyi

Haiwezekani kusiwepo sheria ya fidia kwa wananchi dhidi ya wanyama waharibifu wa mali za wananchi, kwa sasa inaonekana hayo matembo yanaumuhimu kuliko watanzania,,, hii haikubaliki
 
Waruhusu tu trophy hunting. Mali isiwe muhimu kuliko binadamu(mwenye mali).
 
Tembo wamekuwa kero sana katika mikoa ya Arusha, Manyara, Ruvuma, Rukwa, Lindi na Katavi. Halafu wabunge wetu wamekaa kimya tu isipokuwa Nape Nauye. Kwa kweli wabunge wengi hawana uwakilishi unaotakiwa kwa wapiga kura wao. Hawajui majukumu yao.
 
Hili linchi ovyo kabisa
 
Hata Morogoro
 
Back
Top Bottom