Waziri Philip Augustino Mulugo: SIJUI LOLOTE KUHUSIANA NA MITIHANI YA KIDATO CHA SITA INAYOENDELEA

only83

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
5,343
Reaction score
2,527
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, naibu waziri wa elimu katika serikali JK ametoa mpya ya kufungua mwaka baada ya kuulizwa juu ya maendeleo ya mitihani ya kidato cha sita iliyoanza leo. Alipoulizwa na kituo cha EATV kupitia kipindi cha HOTMIX, waziri huyo mwenye historia ya kutofahamu vyema historia ya nchi yake alitoa jibu kuwa....."Sina taarifa yoyote kuhusiana na kuanza kwa mitihani ya kidato cha sita, kwasasa nipo kwenye kikao cha NEC, labda waulizeni waliopo DSM ofisini. Alipoulizwa zaidi aliendelea kusema mimi sijui kuhsuiana na mitihani ya kidato cha sita. Huyu ndie waziri wa elimu ndugu Mulugo.

Source: Hotmix EATV
 
Habari wakuu!

Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi ndugu Philip Mulugo amesema hajui chochote kuhusiana na mitihani ya kidato cha sita iliyoanza nchini kote leo!

Habari hiyo imetangazwa na EATV kwenye kipindi cha Hotmix, kwa mujibu wa EATV ni kwamba Mulugo alitoa kauli hiyo alipopigiwa simu na kituo hicho kutaka kuelezea suala zima la mitihani hiyo ikiwemo maandalizi!

My take:
Inawezekana vipi Naibu waziri unakuwa hujui mambo yanayoendelea katika wizara yako? Je upo hapo kwa ajili ya nini?
 
Kichwani mwake zimejaa kamasi tu,huyo na shukuru ni vilaza wa hali juu mno,sijui kikwete aliangalia sifa gani kwa kuwachagua hawa,mamlaka ya rais yatatutesa yasipo dhitiwa ktk katiba mpya.
 
Tanzania kila kitu kiko kwenye AUTO-PILOT, tuna shida gani!??
 
Bwana Amim ni mtata!..muulizeni mh Sugu
 

eheee hapa waziri tunaye :confused2:
ingekuwa enzi za mwal nafikiri hapohapo angekuwa hana kazi yani waziri unaulizwa kitu kinachohusu wizara tena mitihani ambayo hata iweje waziri lazima utakuwa unajua maana hata kabla ya vyombo kutangaza ama kujua wewe unatakiwa kuwa unajua halafu hujui?
kazi tunayo tanzania
 
tunasafari ndefu sana ya kufika tunakotarajia
 
Naanza kuamini yale maneno kuwa pale wizaran kuna mgogoro kati ya katibu na viongozi wa kisiasa.. Pengine mulugo saiv akienda ofisini ni kusoma magazeti
 
Duh!!! Nimecheka sana hadi machozi yamenitoka sio kicheko cha furaha wala huzuni ila sijajua ni cha nin. Anhaa ni cha hasira kumbe inabidi hili lijamaa liingie kwenye kitabu cha guines
 
upo busy na nec...hayo mengine ya kwenu na watoto wenu...ccm oyeeeer..
 
duh..kaua,inabidi huju jamaa akapimwe na kama akikutwa ni mzima basi akajisajili orijino komedi ndo atafiti.
 

Je ni nani mwenye makosa????????????? wale waliompa kura kuwa mbunge wao au aliyempa madaraka ya unaibu waziri???
 
upo busy na nec...hayo mengine ya kwenu na watoto wenu...ccm oyeeeer..


Hivi hawa mawaziri hawakuhudhuria semina elekezi ya mweshimiwa Rais !? Au walihudhuria lakini kilichoelekezwa hakikueleweka ?
 

Anajua ya SISIEMU-NEC zaidi kuliko kazi yake....simlaumu kwani wa kumlaumu ni JK maana ndiye symbol ya UDHAIFU.
 
Hivi hawa mawaziri hawakuhudhuria semina elekezi ya mweshimiwa Rais !? Au walihudhuria lakini kilichoelekezwa hakikueleweka ?

Yeye hakuhudhuria hiyo, alihudhuria elekezi ya semina kwenye kisiwa cha Zimbabwe..teh..teh..teh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…