Alexander The Great
JF-Expert Member
- Aug 28, 2018
- 4,509
- 23,653
Habari Wana Kijiji,
Binafsi nimeshtuka sana, mpaka nlidodosha bakuli langu la pombe ya kienyeji jana usiku nlipokuwa kilabuni baada ya kupata habari hizi za kuogofya na kushtua.
Habari zenyewe ni baada ya kuambiwa wale jamaa zetu wanaotupa misaada kama taifa, misaada wanayotupa ya kila mwaka tena bila wao kujisifia au kutuzodoa, Wabunge Wa Bunge La Ulaya, ambao Prof Kabudi uliwaita "WAHUNI/WAJINGA" kumhoji Mwenyekiti Wao Wa Bunge kuhusu vigezo alivyotumia kuipa Tanzania msaada ya "€ 27 MILLION" kwaajili ya kupambana na ugonjwa wa Covid-19.
Wakati Serikali ya Tanzania (Ikiongozwa na Mh Rais) kutangaza na kutoa "MAHUBIRI NA MAWAIZA KWA RAIA WAKE" kwamba Tanzania haina ugonjwa huo. Ugonjwa huo ni wa kishetani.
Wabunge Wa Ulaya walikuwa na "HAKI YA KUMHOJI MWENYEKITI WAO" kuhusiana na hizo hela, kwasababu ni hela za walipa kodi wao Ulaya. Hela hizo hawajazokota. Waliwakamua walipa kodi wao. Hela hizo sio kwamba hawakua na kazi nazo, ila kutokana na upendo na heshima waliamua kutupa.
NOTE THAT: Wabunge wale hawakui hoji Tanzania wala hawajakuku hoji wewe kama Waziri Wa Mambo Ya Nje Wa Tanzania. Walimhoji Mwenyekiti Wa Bunge lao.
"MASHARTI YA KUPEWA MSAADA NA MIKOPO" yanajulikana ni lazima "UOMBE KWA KUTOA SABABU ZA MSINGI". Kwa hiyo, sisi kama taifa (Kupitia kwa Wizara Ya Mambo Ya Nje) tuliomba na tulitoa sababu za msingi mpaka kupewa ule msaada na mikopo wa kupambana na Covid-19.
Sasa, uliowaita "WAHUNI/WAJINGA" na kuwatisha kwamba "TANZANIA HAIJAWAHI KUSHINDWA VITA YOYOTE", na wala "HAIJAWAHI KUPIGISHWA MAGOTI KWAAJILI YA MISAADA".
Wameamua kutoa "MAFIGA" na "KUMWAGA CHUNGU CHA MBOGA". Natumai umefurahi sasa kwa ujeuri/ukaidi na dharau uliowafanyia. Sisi kama raia hatukupendezewa kabisa. Sifa ya mtanzania yoyote huwa inajulikana Ukarimu/Heshima/Ukweli/Urafiki/Upendo.
Turudi kwenye mada yangu,
WAHUNI/WAJINGA (Kama ulivyowaita)" wametoa "LIST YA MIKOPO/MISAADA" ambayo sisi kama taifa "TULIOMBA (Narudia tena kwa herufi kubwa TULIOMBA" ili tuweze kupambana na Covid-19. Hawajakurupuka usingizini na kuamua tu kutupa hio misaada. Tuliomba.!!!
Hii kama taifa ni kujivisha "JOHO LA UONGO/UTAPELI NA KUTOKUA WAAMINIFU". Kuomba misaada na mikopo kwa kutumia sababu zisizo za kweli.
BAADHI ya hiyo Mikopo na msaada yenyewe ya kupambana na Covid-19 kama ifuatayo;
1) € 27 Million - Kutoka kwa EUROPEAN UNION (Msaada)
2) $ 143 Million - Kutoka kwa INTERNATIONAL MONETARY FUNDS (Mkopo Mwezi June).
3) $ 3.4 Million - Kutoka kwa WORLD BANK (Mkopo Mwezi September).
4) $ 50.7 Million - Kutoka kwa AFRICAN DEVELOPMENT BANK (Mkopo Mwezi October).
5) $ 11 Million - Kutoka kwa GLOBAL FUND (Mkopo).
KWA UNYENYEKEVU MKUBWA mimi Alexander The Great natoa wito, utoke hadharani na kutupa MAELEZO NA SABABU ZA MSINGI za;
A) Kwanini tuliomba msaada na mikopo ya matrillioni kwa ajili ya kupambana na Covid-19. Wakati Rais alihubiri na kutoa mawaiza kwamba hatuna huo ugonjwa?
B) Hizo hela zilitumika vipi? Na madeni yatarudishwa vipi? Kwa kodi zetu walalahoi?
C) Kwanini uliwatukana na kuwadharau wanaotupa misaada bila sababu ya msingi?
D) Kwanini hujaandika barua ya kuachia nafasi yako kwa maslahi ya taifa?
Ahsante, natumai utaita PRESS YA WAANDISHI WA HABARI WA NDANI NA NJE kutoa maelezo na majibu ya malalamiko yangu.