Waziri Prof. Palamagamba Kabudi, jitokeze na ulieleze Taifa hii mikopo na misaada ya pesa za kupambana na COVID-19 zimetumika vipi

Nimetazama hii video, Nimecheka sana. Ni aibu kwa kweli. Hivi kuna ile pesa ambayo EU walitaka kujua imetumikaje wakati hatukuwa na COVID counter measures. Si ingechukuliwa hivi sasa wanunulie mitungi pale Bugando?

 
Ilijenga Ikulu na Uwanja wa Kimataifa wa Ndege Chato. Nyingine zilitumika kununua wapinzani waliokua viherehere kuhoji hoji hovyo maswala ya hizo hela.

Hela zilizobakia zilitumika kuwalipa posho kina Diamond kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 ambao CCM kwa asilimia kubwa walishinda bila kupingwa na kwa kishindo kweri kweri.

Hela zenyewe zilikua ndogo sana tena ni mikopo (Ambayo tutalipa sisi mpaka wajukuu zetu, ondoeni shaka ndugu wananchi wanyonge), zilikua kama USD Millioni 224.1 tu, pitia hii thread uthibitishe.

 
Hii pesa ameipiga yule jamaa aliyekuwa akinebeba mabunda ya pesa za kuwagawia wadanganyika kwenye ziara uchwara
 
Ilitumika kwenye uchaguzi wa maigizo.

Marehemu alidanganya kuwa uchaguzi tunagharamia wenyewe, lakini ukweli ni pesa kwaajili ya kupambana dhidi ya covid 19 iliyotolewa na taasisi mbalimbali kutusaidia, ilienda kwenye kugharamia uchaguzi hewa.
 
Kama zile Trillion 1.5 hazina jibu mpaka leo sidhani hela hizo watakupa majibu maana ndio hela wanazotumia kununulia wapinzani alafu wananchi ndio walipaji.

Nchi hii jibu sahihi ni kuwatoa majambazi hawa CCM utaona zaidi ya haya.
Alafu mnasema tuchague upinzani,kama kweli upinzani ulikuwa unanunulika kipindi cha Magufuri,basi wapinzani hawafai kabisa,na bora Mungu akuwapa nafasi ya kuongoza nchi maana wangelituuza kabisa.Lowassa aliisha wahi kununua chama chote, kweli wapinza hawana bei.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…