Mkuu 'Shark', HESHIMA kwako.
Kwanza niseme ya kwamba nilipoandika mchango wangu ulioujibu hapa nilikuwa sijaiona hiyo 'clip' uliyoiweka hapo #15.
Ninaheshimu sana mtu anayetoa ushahidi kwa jambo ambalo analiandikia kama wewe ulivyofanya hapa. Jukwaa hili la JF lingekuwa na heshima kubwa sana linapoendesha majadiliano yenye ushahidi, kama hivi ulivyofanya wewe.
Baada ya kuyasema hayo hapo juu, inanipa tatizo sana sasa kumtetea huyu Prof. Mkenda, ambaye kwa hakika niliweka matumaini makubwa juu ya utendaji wake katika wizara hiyo muhimu sana katika maendeleo ya nchi yetu, na hasa katika kuinua maisha ya waTanzania wengi wanaojishughulisha na kilimo.
Kwa hakika hapa Prof. hata sijui nimweleze vipi, ili isionekane kwamba anajiweka katika ku'promote' biashara za kampuni binafsi. Huyu, ingekuwa ni nchi yenye uhuru na haki, ingetakiwa kuwa 'challenged' hata kisheria kwa tabia mbovu ya aina hii anayoonyesha waziwazi.
Hata hivyo, maadam hajazuia mbolea nyingine ziwepo sokoni, uamzi ni wa mkulima binafsi.
Nirudie tena, nakushukuru kwa mchango wako huu wa maana kubwa sana.