Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Waziri wa Ardhi Jerry Slaa amewatia mbaroni watu watatu wakidaiwa kuwa ni matapeli sugu wa Ardhi Wilayani Temeke ambao wamekuwa wakiuza maeneo kadhaa yanayo milikiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kufanikiwa kujipatia Mamilioni ya fedha.
Jerry Silaa amefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao kwa kushirikiana na NSSF baada ya kuweka mtego kama wanunuzi wa ardhi kwa malipo ya Shilingi Milioni nane.
Kufuatia tukio hilo, Jerry Silaa amewataka wananchi kuacha kununua Ardhi chini ya Viongozi wa Serikali za mitaa sambamba na kuwazuia wenyeviti wa Serikali za mitaa kuacha kuuza Ardhi kote nchini
"Ninamtaka Kamishna wa Ardhi nchini kukamilisha mchakato wa kupata stakabadhi ya manunuzi ya Ardhi ambayo itatumika nchi nzima" amesema Waziri Silaa.
Kwa Upande wake Meneja Miliki wa NSSF Geoffrey Timoth, amesema NSSF Ilipokea taarifa ya uwepo wa matapeli wanaohujumu maeneo ya mfuko kwa kuyauza, huku wengine wakivamia maeneo hayo kwa kuamini wataachiwa maeneo hayo na kuongeza kuwa wataanza zoezi la kuvunja nyumba zilizojengwa na wavamizi hao.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa ya Malela kata ya Tuangoma, Wilaya ya Temeke Owing Henry Mkinga, amesema matukio hayo ya utapeli ni ya muda mrefu na yamekuwa yakifanywa na baadhi ya wajumbe wa Serikali ya mtaa, ambapo pia alitumia muda huo kukemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya Viongozi wasio waaminifu
Huu ni mwendelezo wa oparesheni zinazofanywa na Waziri wa Ardhi Jerry Slaa katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi iliyokithiri.