BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Waziri Simba: Tupo makini, tutawashughulikia
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, amesema, si kweli kuwa Serikali inachelewa kutoa uamuzi au haitoi uamuzi sahihi kuhusu vitendo viovu ukiwemo ubadhirifu wa mali ya umma na mikataba mibovu.
Waziri Simba pia amelieleza Bunge kuwa, si kweli kuwa Serikali haikemei vitendo viovu ukiwemo ukiukwaji wa maadili.
Simba amewaeleza wabunge kuwa, Serikali ipo makini kuhakikisha kuwa uamuzi wowote inaoutoa uwe sahihi na wakati mwingine inabidi ifanye utafiti au uchunguzi wa kina kabla ya kutoa uamuzi.
Maamuzi ya Serikali hayawezi kufanywa bila kufanyiwa kazi na bila kuzingatia taarifa zilizopo mikononi mwa Serikali...lengo la kufanya hivyo si kuchelewesha uamuzi bali ni kuhakikisha kuwa uamuzi unaotolewa na Serikali unakuwa ni sahihi, unaozingatia sheria, haki na maslahi ya taifa amesema Waziri Simba wakati anajibu swali la Mbunge wa Kalenga, Stephen Galinoma.
Mbunge huyo amedai kuwa, majibu ya Serikali ni ya nadharia zaidi kuliko vitendo, Waziri Simba amekanusha.
Galinoma pia alimuuliza Waziri Simba ni kwa nini Serikali haikemei maovu na ikasikilizwa kama zamani na kwamba, Serikali haioni kwamba, mambo hayo yanaashiria kuporomoka kwa utawala bora katika taifa letu.
Katika miezi hii ya karibuni taifa limeshuhudia mambo mengi mabaya katika jamii, kwa mfano mikataba mibovu, wizi, na ubadhirifu wa kiwango cha hatari, migomo mbalimbali na matukio ya hapa na pale ya wananchi kujichukulia sheria mkononi amedai Mbunge huyo.
Simba amelieleza Bunge kuwa, matukio mengi ya wizi, ujambazi na uovu mwingine haviashirii kuporomoka kwa utawala bora nchini.
Waziri Simba pia amewaeleza wabunge kuwa, uchu, tamaa, na pupa ya utajiri wa haraka vimesababisha ongezeko la uhalifu nchini. Amesema, uovu huo ikiwemo migomo ni makosa ya jinai yanayofanywa na watu wachache wanaokiuka misingi ya maadili na sheria.
Huu ni uhalifu kama uhalifu mwingine wowote. Serikali itaendelea kupambana nao kwa nguvu zake zote amesema Waziri Simba.
Amesema, Utandawazi umesababisha ongezeko la uhalifu nchini kwa kuwa watu wanaiga tabia na vitendo vya watu wa mataifa mengine.
Kuhusu Mikataba mibovu, na ubadhirifu wa mali ya umma, Serikali na vyombo vyake vinaendelea kuchunguza, kufuatili na kuchukua hatua zinazostahili kwa kuwafikisha mahakamani wale wote watakaobainika kuhusika kwa njia moja au nyingine amesema kiongozi huyo wa Serikali.