Waziri Simba aendeleza usanii katika utendaji wa Serikali

Waziri Simba aendeleza usanii katika utendaji wa Serikali

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Waziri Simba: Tupo makini, tutawashughulikia

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, amesema, si kweli kuwa Serikali inachelewa kutoa uamuzi au haitoi uamuzi sahihi kuhusu vitendo viovu ukiwemo ubadhirifu wa mali ya umma na mikataba mibovu.

Waziri Simba pia amelieleza Bunge kuwa, si kweli kuwa Serikali haikemei vitendo viovu ukiwemo ukiukwaji wa maadili.

Simba amewaeleza wabunge kuwa, Serikali ipo makini kuhakikisha kuwa uamuzi wowote inaoutoa uwe sahihi na wakati mwingine inabidi ifanye utafiti au uchunguzi wa kina kabla ya kutoa uamuzi.

Maamuzi ya Serikali hayawezi kufanywa bila kufanyiwa kazi na bila kuzingatia taarifa zilizopo mikononi mwa Serikali...lengo la kufanya hivyo si kuchelewesha uamuzi bali ni kuhakikisha kuwa uamuzi unaotolewa na Serikali unakuwa ni sahihi, unaozingatia sheria, haki na maslahi ya taifa amesema Waziri Simba wakati anajibu swali la Mbunge wa Kalenga, Stephen Galinoma.

Mbunge huyo amedai kuwa, majibu ya Serikali ni ya nadharia zaidi kuliko vitendo, Waziri Simba amekanusha.

Galinoma pia alimuuliza Waziri Simba ni kwa nini Serikali haikemei maovu na ikasikilizwa kama zamani na kwamba, Serikali haioni kwamba, mambo hayo yanaashiria kuporomoka kwa utawala bora katika taifa letu.

Katika miezi hii ya karibuni taifa limeshuhudia mambo mengi mabaya katika jamii, kwa mfano mikataba mibovu, wizi, na ubadhirifu wa kiwango cha hatari, migomo mbalimbali na matukio ya hapa na pale ya wananchi kujichukulia sheria mkononi amedai Mbunge huyo.

Simba amelieleza Bunge kuwa, matukio mengi ya wizi, ujambazi na uovu mwingine haviashirii kuporomoka kwa utawala bora nchini.

Waziri Simba pia amewaeleza wabunge kuwa, uchu, tamaa, na pupa ya utajiri wa haraka vimesababisha ongezeko la uhalifu nchini. Amesema, uovu huo ikiwemo migomo ni makosa ya jinai yanayofanywa na watu wachache wanaokiuka misingi ya maadili na sheria.

Huu ni uhalifu kama uhalifu mwingine wowote. Serikali itaendelea kupambana nao kwa nguvu zake zote amesema Waziri Simba.

Amesema, Utandawazi umesababisha ongezeko la uhalifu nchini kwa kuwa watu wanaiga tabia na vitendo vya watu wa mataifa mengine.

Kuhusu Mikataba mibovu, na ubadhirifu wa mali ya umma, Serikali na vyombo vyake vinaendelea kuchunguza, kufuatili na kuchukua hatua zinazostahili kwa kuwafikisha mahakamani wale wote watakaobainika kuhusika kwa njia moja au nyingine amesema kiongozi huyo wa Serikali.
 
Waziri Simba: Tupo makini, tutawashughulikia
Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 29th January 2010
Habari Leo

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, amesema, si kweli kuwa Serikali inachelewa kutoa uamuzi au haitoi uamuzi sahihi kuhusu vitendo viovu ukiwemo ubadhirifu wa mali ya umma na mikataba mibovu.

Waziri Simba pia amelieleza Bunge kuwa, si kweli kuwa Serikali haikemei vitendo viovu ukiwemo ukiukwaji wa maadili.

Simba amewaeleza wabunge kuwa, Serikali ipo makini kuhakikisha kuwa uamuzi wowote inaoutoa uwe sahihi na wakati mwingine inabidi ifanye utafiti au uchunguzi wa kina kabla ya kutoa uamuzi.

“Maamuzi ya Serikali hayawezi kufanywa bila kufanyiwa kazi na bila kuzingatia taarifa zilizopo mikononi mwa Serikali...lengo la kufanya hivyo si kuchelewesha uamuzi bali ni kuhakikisha kuwa uamuzi unaotolewa na Serikali unakuwa ni sahihi, unaozingatia sheria, haki na maslahi ya taifa” amesema Waziri Simba wakati anajibu swali la Mbunge wa Kalenga, Stephen Galinoma.

Mbunge huyo amedai kuwa, majibu ya Serikali ni ya nadharia zaidi kuliko vitendo, Waziri Simba amekanusha.

Galinoma pia alimuuliza Waziri Simba ni kwa nini Serikali haikemei maovu na ikasikilizwa kama zamani na kwamba, Serikali haioni kwamba, mambo hayo yanaashiria kuporomoka kwa utawala bora katika taifa letu.

“Katika miezi hii ya karibuni taifa limeshuhudia mambo mengi mabaya katika jamii, kwa mfano mikataba mibovu, wizi, na ubadhirifu wa kiwango cha hatari, migomo mbalimbali na matukio ya hapa na pale ya wananchi kujichukulia sheria mkononi” amedai Mbunge huyo.

Simba amelieleza Bunge kuwa, matukio mengi ya wizi, ujambazi na uovu mwingine haviashirii kuporomoka kwa utawala bora nchini.

Waziri Simba pia amewaeleza wabunge kuwa, uchu, tamaa, na pupa ya utajiri wa haraka vimesababisha ongezeko la uhalifu nchini. Amesema, uovu huo ikiwemo migomo ni makosa ya jinai yanayofanywa na watu wachache wanaokiuka misingi ya maadili na sheria.

“Huu ni uhalifu kama uhalifu mwingine wowote. Serikali itaendelea kupambana nao kwa nguvu zake zote” amesema Waziri Simba.

Amesema, Utandawazi umesababisha ongezeko la uhalifu nchini kwa kuwa watu wanaiga tabia na vitendo vya watu wa mataifa mengine.

“Kuhusu Mikataba mibovu, na ubadhirifu wa mali ya umma, Serikali na vyombo vyake vinaendelea kuchunguza, kufuatili na kuchukua hatua zinazostahili kwa kuwafikisha mahakamani wale wote watakaobainika kuhusika kwa njia moja au nyingine” amesema kiongozi huyo wa Serikali.

Mimi bwana huyu mama akisema siku hizi, huwa sitoi comments. JK alipokwenda Same kuwapa pole watu kwa mafuriko, alisema; Anna Kilango unaisema sana serikali yangu...!. Hiyo ni muda mfupi baada ya Sofia Simba kulipuka kuhusu Anna Kilango kwenye kamati ya Mwinyi kwamba Ana Kilango anapiga kelele kwa sababu kaukosa U-first lady na.....! Kauli ya JK ilikuwa mwangwi wa maneno ya Sofia Simba kwa kamati ya Mwinyi.

Kwenye suala la kuongoza serikali, kama kuna issue tata yoyote, njia nzuri ya awali kuitatua ni kwa wahusika wakuu kujiuzu. Iwapo wahusika wakuu hawajiuzu, mbali ya kutochukuliwa sheria, inatia shaka sana sana. Hata kama hawahusiki moja kwa moja, kuachia ngazi ndiyo utawala bora Duniani kote. Mimi ningekuwa Galinoma, ningemwambia wazi Waziri kuwa: Lowasa, Karamagi, Msabaha, Mwakapugi, Manyika na mwenyekiti wa board ya Tanesco by then wajiulu instantly. Achilia mbali chenge na wenzake.

lakini ndiyo siasa.
 
- Mkuu hoja yako nzito sana, ila unahitaji kuimaliza yote, maana Sophia ile siku alisema maneno mengi sana, sasa ni vyema ukatuhakikishia kwamba yote yalikuwa ni mwangwi wa JK kama unavyosema, ninaomba unisaidie kuelewa kwamba aliposema kwamba Lowassa ndiye mwanaume wa shoka katika viongozi wote wa Tanzania ulikuwa ni mwangwi wa JK, au?

Kwenye suala la kuongoza serikali, kama kuna issue tata yoyote, njia nzuri ya awali kuitatua ni kwa wahusika wakuu kujiuzu. Iwapo wahusika wakuu hawajiuzu, mbali ya kutochukuliwa sheria, inatia shaka sana sana. Hata kama hawahusiki moja kwa moja, kuachia ngazi ndiyo utawala bora Duniani kote. Mimi ningekuwa Galinoma, ningemwambia wazi Waziri kuwa: Lowasa, Karamagi, Msabaha, Mwakapugi, Manyika na mwenyekiti wa board ya Tanesco by then wajiulu instantly. Achilia mbali chenge na wenzake.

lakini ndiyo siasa.

- Wananchi wengi wa Shinyanga waliuliwa kwa sababu ya kushukiwa kwamba ni wachawi bila ushahidi wa klutosha mbele ya sheria, Mwinyi akajiuzulu na baadye kwua Rais, infact tuliambiwa na wapiga debe wake kwamba kujiuzulu kwake kulikuwa moja ya strength zake kama kiongozi,

- Sasa naomba kukuuliza kujizulu kwa Mwinyi kulisaidia nini wananchi waliopoteza their loved ones kwenye kushukiwa? My point ni kwamba dawa ni kufikishana kwenye sheria sio kujiuzulu tu! Lowassa si alijiuzulu so what?

Respect.

FMEs!
 
Back
Top Bottom