kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Waziri Simbachawene amemwagiza IGP kuwaondoa trafiki wote wenye vitambi na kuwapangia kazi nyingine.
Najiuliza, ipo sheria inayokataza trafiki kuwa na kitambi? Shughuli ya utrafiki Ni ngumu kuliko majukumu ya OCD, OCS na RPC?
Natamani awamulike pia hao, ila pia tofauti na utrafiki kazi zilizobaki polisi zote ngumu na nzito hivyo sidhan Kama Kuna kitengo kinachofaa zaidi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Geogre Simbachawene, amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, kuwaondoa askari wa Usalama Barabarani wenye vitambi na kuwapangia kazi nyingine kwani wamekosa sifa. Ametoa kauli hiyo wakati wa Kongamano la Usalama Barabarani lililofanyika jijini Dodoma lililoandaliwa na TAMWA kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia zinazochochea mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973.
"Wapo trafiki wanastahili kuondolewa kwa kukosa sifa ya kuwa trafiki! Kwa mfano wa trafiki wa Gairo wana vitambi! Askari anakuwaje na kitambi? Namuagiza IGP kuwaondoa askari wote wenye vitambi na kuwapangia kazi nyingine, amesema Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene ameongeza kwa kusema kuwa wapo askari wasio waadilifu wanaotumia sare na kofia zao kula rushwa. "Wapo askari wa usalama barabarani ambao wamegeuza 'crown', sare nyeupe na kofia kudai rushwa kutoka kwa bodaboda, malori na kirikuu!! Naelekeza trafiki kufanya kazi kwa weledi! tuache kusimamia sheria kwa mazoea!”, amesisitiza
Amesema kuwa ajali zimekuwa zikigharimu serikali kurekebisha miundombinu, kufanya uokozi na kupoteza nguvu kazi ya taifa. "Ajali hizi zimekuwa zikiigharimu serikali kurekebisha miundombinu, kufanya maokozi na kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Vilevile, Waziri Simbachawene amesema kuwa wapo madereva wanaendesha magari wakiwa wamelewa; wapo watembea kwa miguu wanavuka barabara wakiwa wamelewa; wapo madereva wanaendesha mwendokasi hatarishi katika maeneo ya makazi ya watu au yasiyoruhusiwa na alama za barabarani.
Katika kongamano hilo Waziri Simbachawene aliahidi kwamba mapendekezo hayo ya maboresho ya Sheria yaliyotolewa na wadau yatapelekwa Bungeni baada ya mchakato ndani ya Serikali kukamilika. "Serikali kupitia wizara yangu ipo katika mchakato wa kurekebisha Sheria ya Usalama Barabarani 1973, ili iweze kuendana na mahitaji ya sasa", amesema Simbachawene
"Kongamano la usalama barabarani ni siku muhimu sana ya kukumbushana kuhusu masuala mbalimbali ya usalama barabarani. Masuala hayo ni pamoja na kuwakumbusha madereva juu ya kuwa waangalifu na kuzingatia sheria", amehitimisha Waziri Simbachawene.
Ripoti ya usalama barabarani ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) iliyotolewa mwaka 2018, inabainisha kuwa Sheria za Tanzania zina upungufu katika kudhibiti usalama barabarani, ikiwemo kuruhusu kiwango kikubwa cha ulevi kwa madereva bila kujali uzoefu wa dereva katika kazi husika.
Tanzania imeweka ukomo wa kilevi kuwa ni 0.08g/dl lakini WHO inaeleza kuwa dereva mwenye kiwango hiki cha ulevi anakua hatarini kupata ajali mara nne zaidi ya yule ambaye hajatumia pombe kabisa. WHO pia wanashauri kuwa ni vizuri ukomo wa ulevi ukawa ni 0.05g/dl kwa madereva wazoefu na 0.02g/dl kwa madereva wapya wasio na uzoefu.