Polisi waendelee kuajiri hao wanaodhaniwa wana elimu ndogo, kwani suala elimu kubwa na ndogo ni mchakato tu wa kupata fursa ya kusoma, kuna ambao wanatamani kupata elimu ya chuo kikuu lakini kutokana mchakato wake kuwa na vikwazo na vizuizi vingi kitaaluma wengi huishia njiani,
hawafiki elimu ya juu inayotakiwa hasa. Haijulikani kuna siri gani elimu ya juu kuchagua wachache ikiwa wengi wanaitaka elimu hiyo.
Ifahamike kuwa mwanafunzi haendi shuleni\chuoni kufeli, kule ni kupata maarifa na stadi tu, haya matokeo na upuuzi mwingine kutangaziana kufeli na kufaulu ni namna tu ya kupata idadi ndogo ya watakaoruhusiwa kuendelea na masomo ya juu.
Hata hawa wanaoachwa bado wana akili nyingi kupata ajira wanayoomba. Usomi ni kupata taarifa, stadi na maarifa ya kufanya kazi fulani na kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Kwa hiyo hakuna askari mwenye elimu kubwa na ndogo katika utekelezaji wa majukumu yao. Vyeo walivyo navyo ni itifaki tu ili kazi ifanyike kwa ufanisi na weledi.