Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Miaka ya themanini baada ya vita vya Kagera mikoa ya kanda ya ziwa ilishuhudia wimbi kubwa la uvamizi wa kutumia siraha.
Nilikuwa najitambua japokuwa nilikuwa mdogo kiumri. Mtaa na kijiji nilichoishi alikuwepo mzee mmoja alikuwa na uwezo kidogo na kila mtu alitambua kuwa alikuwa akimiliki gobole au shotgugun. Maana alikuwa akienda kuwinda nalo na pia alionekana mara kwa mara akilibeba ili kwenda nalo kulipia leseni.
Siku moja miaka ya 1980's majambazi walivamia kwenye mji wa jamaa mmoja jina nalihifadhi ambae alikuwa na maduka ya bidhaa toka Kenya. Maana miaka hiyo kila kitu maneo ya kanda ya Ziwa zilitumika bidhaa toka Kenya. Na majambazi hayo yalitishia wananchi kwa kupiga baruti ili yaonekane yana siraha za moto.
Hakuna aliyepata ukweli juu nini kiliporwa hapo kwenye hilo tukio. Lakini kesho yake kila mtu alikuwa na swali moja tu. Mzee Machemba alikuwa wapi kulinda jamaa zake maana yeye ana gobole ambalo linaweza kulinda mtaa na kijiji.
Hatukusikia mzee Machemba akifyatua hata warning shot ili majambazi watimue mbio.
Leo hii tunambiwa na Igp Sirro tuwe na mapanga ili kujilinda. Hivi yatawatisha majambazi walio na Ak 47? Kama hata hatuna gobole kama la mzee Machemba?