Waziri Simbachawene umedharau kauli ya Spika?

Walimu wa kujitolea ni sawa na "tegesha"wapo pale kusubiri huruma katika ajira. Ndio hao wanaolalamika humu. Hongera Mh. Waziri ajira ni haki ya kila muombaji na sio kikundi cha tegesha pekee.
Na ukitaka kuamini unachosema Mkuu wape interview,hutoona tofauti yoyote ya maana baina ya anaejitolea na ambae hajitolei ndo maana wakiskia interview wanalia Lia......kibaya zaidi hizo nafasi zenyewe za kujitolea juwa wanapata kimagumashi isipokuwa kwa wachache sana
 
. Kujitolea ni ujinga wako mwenyewe,

. Watu kama nyinyi mnaojitolea inatakiwa msiajiriwe kabisa mpaka mnazeeka/vikongwe. 🤒🤒
 
Mtu kamaliza chuo 2015 mpaka saivi hola, unategemea mtu huyo awe anajitolea tuu ili apewe kipaumbele cha ajira?
 
Nimeona unene wa mawazo yako.
 
Ha ha ha
 
Unajitolea kwenye taasisi kama nani?
Sio jukumu lako kutoa msaada wa kufundisha ni jukumu la serikali kuhakikisha inatoa elimu bora kwa kuajiri raslimali watu.

Kama msomi bado unadanganywa hivyo basi hata Elimu yako haijakusaidia. WFK
Siandike kutafuta huruma bali uhalisia wa mambo
 
Kabisa aisee
 
Hii hoja ni dhaifu sana na ikienda mbali zaidi kwenye taasisi nyingine za serikali italeta undugu kwenye ajira.

.........Tunajua ili upate nafasi ya kujitolea kwenye baadhi ya taasisi na Halmashauri lazima uwe na ndugu wa kukushika mkono kwahiyo mnataka kazi zikitoka hao wanaojitolea wenye ndugu huko ndio waendelee kupata kazi serikalini.

..........Mh. Spika hizi kazi za serikalini acha watu wapambane kwa usaili tu kila Mtanzania ana haki ya kuzipata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…