Waziri Simbachawene, Zitto akamatwe na kulisaidia jeshi la polisi kumpata kijana aliyempa taarifa kuwa hayati Magufuli alituma watu kuchoma mali zake

Kwa nini kama ana taarifa akamatwe au ukiwa na taarifa za uhalifu mpaka ukamatwe? Kama hivyo ndivyo, nani yuko tayari kukamatwa ili atoe taarifa? Kama anaona inatakiwa angesema 'Zitto awasaidie polisi kupata taarifa kuhusu kuchoma shamba lake'.
 
Hakuna shaka kwamba marehemu pombe alikuwa na matendo kama hayo hata zaidi... Japo zito ni mnafiki lakini katika hili hamna shaka
Mashamba ya Mbowe kule hai yaliyoharibiwa chini ya biyakanwa na yakawe mfano kuthibitisha hili!
Jitu halijawahi hata kuwa mwalimu mkuu wa shule linapewa nchi?
 
Kuna chuki za aina ngapi kwani?

Nitaandika kuhusu uhalifu wa Magufuli hadi siku yangu ya mwisho ya kupumua. Yaani yule muuaji na mwizi ndiyo mnalazimisha aonekane katenda mema ya ajabu Tanzania. HAPANA
Kiongozi mwizi na muuaji angekubalika namna hii kwa kutetea maslahi ya umma.
 
Ulichoandika kina mahusino na Zitto kusaidia polisi kuwajua waliotumwa na JPM kuchoma mali za Zitto?
We Nyankurungu hivi ni kweli hauoni uhuiano wa maelezo ya saint ivuga na kumkamata mchomaji wa mashamba na majengo? Au ni we ni mshirika/ mnufaika wa matukio hayo?

Ni hivi, hoja ya saint ivuga anahoji kuwa kama ninyi washirika wa Jpm mlikuwa wapi wakati huo mkashindwa huwaita mwahoji waliochoma ofisi za imma advocates, mashamba ya Mh Mbowe na Mh Zitto, nyumba nk huku wahanga wa matukio wakijibiwa maneno "mbofu mbofu" kuwa wanatafuta umaarufu.

Kwa sasa mkae kimya muache watu wasikie lolote linaloweza kusemwa pengine wanaweza pata fununu za watesi wao maana wakati huo hamkuona umuhimu wa kufanya uchunguzi hata wa wale waliopigwa risasi na kuokotwa katika viroba.
 
Mbona unapanic?
Simbachawene hana IQ ya kutusha kumsaidia yeye wala serikali anayoitumikia.
Utafikiri haoni hii aibu serikali inayoibeba kwenye kesi ya Mbowe.

Wengine tunaona ni sawa tu, akamatwe apelekwe mahakamani ili tusikie vitimbwi vya wasiojulikana.

Hatimaye tulijua tu watajitokeza na kujua waliowatuma.
 
Acha kuongea pumba, ushirika na JPM kisa tu kutaka Zitto aeleze wailiompa taarifa za JPM kutuma watu wachome nyumba zake?

Mashamba ya Mbowe yanaingia vipi? Hujui sheria ya mazingira?

Zitto kaibua hoja, anatakiwa awa a aidie polisi kuwapata wahalifu
 
Hawawezi Kumkamata Kwa Sababu wanajua Jinsi Mwendakuzimu alivyokuwa Ibilisi
 
Kiongozi mwizi na muuaji angekubalika namna hii kwa kutetea maslahi ya umma.
Hata Adolph Hitler huko Germany kuna watu wanamkubali hadi leo na kuna siku maalum wanaandamana na kufanya kumbukumbu yake. Huyu Mwendazake anakubalika na wasio na kisomo aliiwabatiza jina "wanyonge".

Mwenye akili timamu ukimuita mnyonge, mtagombana
 
Huu mfano wa Hitler sio relevant.
 
Utakamata wangapi kwa ajili ya kumsafisha DIKTETA wa Chato? Kitu gani wewe unatia wasiswasi juu ya UFEDHULI Magufuli?

Huhitaji kumkamata Zitto kujuwa kuwa Magufuli alikuwa SHETANI. Mambo yote yako kwenye clips zake akiagiza
Mkuu mbona makasiriko sana au kwa vile alikufukuza kazi yako ya askari magereza
 
Vipi yule aliyemuua Akwilina Akwilini kwa risasi ya kukata kona
 

Siasa za JIWE zilikuwa za Hovyo sana ,unashangaa kuchomewa shamba na nyumba? Mbona ni ndogo sana hizo ,ulijiuliza wale waliokutwa kwenye viroba? Ben, Azory, Kanguye, Rujabe wamepotea!!
 

Magufuli alikuwa Rais muhalifu na alifanya matendo mengi ya kihalifu, ila tuna katiba inayolinda marais wahalifu. Lakini hakuna shida iko siku hizi kinga zitaondolewa. Pamoja na kwamba Zitto ni mnafiki ila kwa hili ameongea ukweli.
 
Magufuli alikuwa rais muhalifu, na alifanya matendo mengi ya kihalifu, ila tuna katiba inayolinda marais wahalifu. Lakini hakuna shida iko siku hizi kinga zitaondolewa. Pamoja na kwamba Zito ni mnafiki ila kwa hili ameongea ukweli.
Wewe unajulikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…