GE2025 Waziri Stergomena Tax: Maafisa Usafirishaji nyie ni watu muhimu sana. Mna mchango mkubwa katika kutunza amani

GE2025 Waziri Stergomena Tax: Maafisa Usafirishaji nyie ni watu muhimu sana. Mna mchango mkubwa katika kutunza amani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa JKT, Mhe. Dkt. Stergomeana Tax, amewataka maafisa usafirishaji kwa njia ya pikipiki (bodaboda), kote nchini kuwa mabalozi wazuri wa kulinda amani ya nchi, hususani katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu wawapo katika shughuli zao kwani wanakutana na kuwahudumia watu wengi hivyo watumie fursa hiyo kutokubali kurubuniwa na kujiepusha na vitendo vya uhalifu.

Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax, ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na kufanya kikao na viongozi wa maafisa usafirishaji kwa njia ya pikipiki (bodaboda) wakiwawakilisha kundi kubwa la bodaboda Wilaya Magu, mkoani Mwaanza, kikao ambacho kimetokana na maombi ya mara kwa mara ya viongozi wa bodaboda kuomba kukukutana na kuzungumza na waziri Dkt. Tax. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, wilayani Magu ndugu Fratha Andrea Katumwa.



WhatsApp Image 2025-09-21 at 12.43.43_2716ab11.jpg

WhatsApp Image 2025-09-21 at 12.43.43_7312d016.jpg
 
Back
Top Bottom