Waziri Tax: Hakuna malimbikizo kwa wastaafu wanaohusiana na JWTZ

Waziri Tax: Hakuna malimbikizo kwa wastaafu wanaohusiana na JWTZ

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Akijibu swali la Mbunge Esther Matiko aliyehoji kuhusu uwepo wa malalamiko ya Wastaafu kucheleweshewa mafao yao kutokana na sababu mbalimbali, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax amesema Wastaafu wanaohusiana na Wizara yake hakuna malimbikizo na wanaendelea na uhakiki.

Awali, Agosti 11, 2023, Mdau aliyejitambulisha kuwa ni Mstaafu wa Jeshi aliomba Rais Samia Hassan Suluhu kuwasaidia akidai wamekuwa wakifuatilia mafao ya Kiinua Mgongo bila mafanikio, akitoa mfano malipo ya Mifuko ya Hifadhi alitumikia Miezi 495 lakini malipo ya stahiki aliyopata ni ya Miezi 272.

Pia, Mei 20, 2024, Mdau mwingine alishauri Serikali ishughulikie changamoto za mafao na stahiki za Wastaafu wa Vyombo vya Usalama akidai kumekuwepo na vilio vingi kuhusu kutotimiziwa stahiki zao.

Pia soma:
~ Vilio vya Wastaafu wa majeshi vitatuliwe haraka, kinachoendelea ipo siku kitatengeneza ‘matunda yasiyofaa’
~ Rais Samia, Watumishi Wastaafu wa Jeshi tunaomba utusaidie kupata stahiki zetu, tunateseka
 
Hayapo na wanaendelea kufany utafitii, ni vyema mkaharakisha kama serikali , ila kama raia na mlipa kodi naomb kuhoji mna fanya utafiti wa kitu ambacho mmekiri kuwa hakipo?
 
Back
Top Bottom