Waziri Ummy: Changamoto kubwa inayowakabili Watanzania kupata Huduma za Afya ni gharama

Waziri Ummy: Changamoto kubwa inayowakabili Watanzania kupata Huduma za Afya ni gharama

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kuwa changamoto kubwa inayowakumba Watanzania katika kupata huduma za afya ni gharama kuwa juu, hivyo amesisitiza wadau kuwahamasisha kuwa na bima ya afya ambayo amedai kuwa itawawezesha kupata matibabu kwa urahisi.

"Ukiwauliza Watanzania leo changamoto kubwa inayowakabili katika kupata huduma za afya watakwambia ni gharama.

"Kama kweli tunawapenda kweli Watanzania tuwahamasishe na kuwahimiza kuwa na bima ya afya ili waweze kupata matibabu kwa urahisi kabla ya kuugua," amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Pia Waziri Ummy amesema kuwa kuna watu wamekuwa wakiuza mali zao akitolea mfano nyumba ili kugharamia matibabu, kufuatia hali hiyo amesema kuwa Serikali inalichukulia kwa uzito mkubwa suala la bima ya afya kwa kuwa inalenga kuwezesha watanzania kupata huduma bila vikwazo.

"Tuna ushahidi wa kesi za watu wanaouza nyumba zao ili waweze kugharamia matibabu. Kwetu sisi Serikali kupitia Wizara_afya, bima ya afya tunaichukulia kama ukombozi kwa Mtanzania kwa sababu atapata uhakika wa kupata matibabu bila vikwazo," amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Ameongeza kuwa: "Bima ya afya ni kwa ajili ya kumsaidia Mtanzania hususani masikini, kwa sasa Mtanzania masikini akiumwa atauza mali zake alizonazo ili apate matibabu, wapo wanaouza pikipiki, viwanja ili tu kumudu gharama za matibabu."

Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo Januari 23, 2023 wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, huku ikiwa zimepita siku chache tokea Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, John Heche kutoa kauli akiwa Mkoani Mwanza kwenye uzinduzi wa mikutano ya hadhara Januari 21, 2023 akidai kuwa changamoto kubwa ya watanzania kwa sasa ni uhitaji wa huduma bora ya afya kuliko uhitaji wa bima ya afya.

Alieleza kwa kuhoji juu ya suala la upungufu wa Watumishi wa afya pamoja na vituo vya afya akidai kuwa hilo ni tatizo lililopo kwa sasa.



Upungufu wa madaktari bingwa na wabobezi
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema: “Wizara ya Afya ilijiwekea lengo la miaka mitano (2020-2025) la kusomesha wataalamu bingwa na Wabobezi wasiopungua 300 kila mwaka na kuwa kipindi cha 2020/21 na 2021/22 tumesomesha wataalamu bingwa 524 ambao wanaendelea na masomo ndani na nje ya Nchi

“Amesema lengo ni kuimarisha huduma ya matibabu kupunguza rufaa za wagonjwa nje ya Nchi

“Tumefanya uchambuzi hadi kufikia Desemba 2021 na kubaini mahitaji ya madaktari bingwa katika hospitali za Serikali zinazotoa huduma za kibingwa na kibobezi ni 1782 wakati wataalam ambao wamesomeshwa na Serikali ni 992, hivyo bado tuna pengo kubwa la waaalam hao.”
 
Sasa waziri Ummy anamlalamikia nani?

Chadema imesema wizara ya afya Ina tatizo la kutoa huduma ya afya. Inahoji kuwa ; bima itatoa huduma ya afya?
 
wabobezi bila kuweka scale za mishahara ni time wastage masters ina tosha kuishi mjini
 
Sasa waziri Ummy anamlalamikia nani?

Chadema imesema wizara ya afya Ina tatizo la kutoa huduma ya afya. Inahoji kuwa ; bima itatoa huduma ya afya?
Walivamia sera ya plbima ya afya kwa bila kujua msingi wale. Tumewapiga chenga😁😁
 
Back
Top Bottom