Waziri Ummy: Inasikitisha madaktari kuombana rushwa

Waziri Ummy: Inasikitisha madaktari kuombana rushwa

Willima

Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
26
Reaction score
39
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema rushwa imekithiri na kuota mizizi katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) kiasi cha madaktari kuombana rushwa wenyewe kwa wenyewe.

Ummy aliyasema hayo juzi, alipozindua bodi mpya ya wadhamini wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) akiwa na viongozi waandamizi wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo.

“Kati ya hospitali mbili ambazo nalala usingizi ni JKCI na Benjamin Mkapa ya Dodoma. Ni kati ya hospitali za Serikali zinazofanya vizuri. JKCI huwezi kusikia malalamiko ya hovyohovyo kutoka kwa wagonjwa, ikiwamo uombaji rushwa. Nimekaa Wizara ya Afya miaka mitano na sasa nina miezi sita sijawahi kusikia mgonjwa ameambiwa sijui leta hela au anazungushwazungushwa,” alisema na kuongeza:

“Nawaagiza waganga wafawidhi nendeni mkajifunze JKCI, (Profesa Mohamed) Janabi anafanya kitu gani. Benjamin Mkapa nako hakuna malalamiko ya hovyohovyo ila MOI panasikitisha…yaani daktari anamuomba rushwa daktari mwenzake, imefikia hatua mpaka wanaanikana kwenye magrupu kwa mtaalamu mwenzie kumuomba rushwa halafu huyo mtu analipwa mshahara, wanachukua asilimia 70 ya fedha za NHIF lakini nisiharibu mkutano nitaenda kusema nikifike kule."

MWANANCHI.
IMG_20220805_094454.jpg
 
JKCI wanalipwa vizuri, wana allowances kama zote na zinalipwa on time.... Ila kwingineko ni majanga na bila kuiga mfumo wa uendeshaji wa JKCI hospitali za umma zitaendelea kuwa hovyo, sio MOI tuu..
 
Back
Top Bottom