itakua wizara ya afya nayo ina matatizo ya afya ya akili!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga. Kitengo cha magonjwa ya akili wanauzia wagonjwa dawa kwa Bei ya juu sana
Nina mgonjwa wangu huwa nampeleka kuchua dawa hapo, mwezi uliopita nilinunua dawa kwa shilingi 11,000 juzi nilienda mhimbili naambiwa dawa 54,000, na ni dawa hizo yaani carbamazipine na phenegan.
Nilichoambiwa kwamba dawa za phenegan zimepanda kwamba kidonge kimoja shilingi Mia tano, na cha ajabu nakuja kuuliza maduka ya Kariakoo naambiwa dawa ni shilingi 50, Mh. Waziri ni kweli dawa zimepanda kiasi hicho au tunaibiwa wenye wagonjwa.
Sidhani kama wanaliona hilo maana hawajichanganyi na wananchi waoHuku barabarani wagonjwa wa akili ni wengi sana serikali ilitambue hilo
Ova
Ndugu acha kukariri, siyo magonjwa yote yanatokana na bangi.Acheni bangi zinaharibu afya ya akili
Zamani hzi dawa zilikua zinatolewa bure, lakini Cha kushangaza watu wa methadone(wale wanaotumia madawa ya kulevya ndio wanatibiwa bure). Wengonjwa wengine wanalipa. Serikali Angalieni hili.Wengine hatuna uwezo wa kukata BimaSidhani kama wanaliona hilo maana hawajichanganyi na wananchi wao