vipik2
JF-Expert Member
- Nov 24, 2011
- 2,845
- 2,258
Dawa ndogo tu, ma DED wote wawe akina Mama na akina dada.
Hapo sasa utaongeza akina" Marioo" mtaani ambao watakuwa na vita na bodaboda kila siku
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dawa ndogo tu, ma DED wote wawe akina Mama na akina dada.
Hutobaki kama mkeo akiwa miongoni mwa wanaopiganaUkimwi utusaidie, Maccm yamfuate Mwenyekiti.
Kwanza umeandika nini hapo mkuu, hivi unahisi wewe huwezi kuupata huo ukimwi.Ukimwi utusaidie, Maccm yamfuate Mwenyekiti.
Morogoro muacheni my wanguNa sisi huku wanaume tunapigana kisa ded mmoja hapa morogoro (aliyepata ajali nadhani mnamjua)
Ccm ni wazinzi na waasheratiWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, amedai kuwa amebaini kuwapo wakurugenzi wanaume kutumia vyeo kujihusisha kimapenzi na watumishi wa kike.
![]()
Amesema tabia ya wakurugenzi hao inasababisha baadhi ya watumioshi kupigana kwa sababu yao.
Aidha, amewapa tumbo joto wakurugenzi wapya 61 wa halmashauri walioteuliwa, hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaambia kuwa wako chini ya uangalizi kwa miezi sita wakipimwa utendaji kazi wao.
Waziri Ummy aliyasema hayo jana kwenye mafunzo elekezi kwa wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa nchini na kusisitiza, kuwa hatavumilia uonevu na udhalilishaji, dhidi ya wanawake kwa kisingizio cha cheo cha ukurugenzi.
“Mimi Waziri ninayemsaidia Rais sitavumilia suala hilo. Sasa umekuwa mkurugenzi kila mfanyakazi mzuri kwenye halmashauri yako ni wako. hii hapana.
"Hili ni moja ya mada Katibu Mkuu atalisema hapa. Hatuwezi kwenda hivyo hawa ni binadamu lakini tunazo kesi wakurugenzi wanasababisha watumishi wanawake wanapigana kisa mkurugenzi. Mtu wa aina hii hafai wala hatoshi kuwa mkurugenzi," alisema huku akisema bado hajapata kesi za wakurugenzi wanawake.
"Sijapata kesi za wanawake, lakini wanawake wenzangu twende tukajiheshimu. Hii ni nafasi kubwa sana, siyo leo upo na huyu, kesho na huyu haileti taswira nzuri kwa kiongozi wa umma katika nafasi," alisema huku akiwataka wakurugenzi wanawake kulinda utu na heshima waliyopewa na rais na kuangalia watu wanaotoka nao kimapenzi.
"Kuna mwingine ametongozwa amekataa basi hapelekwi semina. Anahamishwa kisa amemkataa mkurugenzi. Hebu tafuta nje ya halmashauri, lakini isiwe chanzo cha wanawake kupigana maana posho nayo huwa kubwa unajengewa nyumba, wanapewa gari inabidi wanawake tu wapigane,"alisema.
Kuhusu wakurugenzi wapya, Waziri Ummy alisema wako chini ya uangalizi kwa miezi sita na wanapaswa kuonyesha uwezo wao, kwenye utendaji kazi kwa kuwa waliteuliwa kwa kuangalia wasifu na utendaji kazi wao, maeneo waliyokuwapo awali.
“Niseme bila kupepesa macho, mpo kwenye uangalizi na tutapima utendaji wenu kwa sababu mliteuliwa kwa kuangalia, CV (wasifu) na utendaji wa huko mlikokuwa. Sasa kwenye kazi ya ukurugenzi ni watu ambao mtamsaidia Rais Samia kusimamia shughuli za utawala na maendeleo kwenye mamlaka za serikali za mitaa. Hatuwatishi mpo kwenye uangalizi baada ya miezi sita mimi na Naibu Mawaziri, Katibu Mkuu tutapeleka taarifa kwa rais, atafanya uamuzi,” alisema.
Pia aliwataka wakurugenzi wa zamani, ambao wameaminiwa tena kuongeza kasi ya utendaji kazi, huku akisema wengine wamerudi baada ya Rais Samia kuona awape nafasi tena.
“Mheshimiwa rais ameona asihukumu, labda kulikuwa na changamoto, kwa hiyo hii ni second chance, lakini kubwa ni imani kubwa kwa rais kwetu, mafunzo haya ni ya kukumbushana namna ya kutekeleza majukumu yetu kwenye mamlaka za serikali za mitaa,”alisema.
Alisema ni wakati wao kuonesha uwezo wao wa kiutendaji kwa Mamlaka ya uteuzi na watapimwa kwa matokeo ya kazi zao.
Pia alisema amepokea kesi za wakurugenzi kugombana na wenyeviti wao na kuwataka kutumia mafunzo hayo kujiepusha na migongano hiyo.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof. Riziki Shemdoe, alisema hadi juzi kuna halmashauri 22, ambazo hesabu zao hazijasomeka, kwenye mfumo wa fedha wa serikali.
Alitaja Halmashauri hizo kuwa ni Jiji la Dar es Salaam, Bahi, Mvomero, Newala, Newala TC, Chalinze, Kibaha, Songea, Madaba, Itilima, Manyoni, Songwe, Muheza, Bumbuli, Kilindi, Kishapu, Msalala, Shinyanga, Kahama na Lushoto.
Alikua ni DAS yule sio DED...Nimekumbuka ya Kidoti na yule jamaa angu DED.
Shujaa hakumuacha salama.
Hawaelewi ndugu na watawaoa haohao.Liverpool VPN umelizungumzia hili sana humu na hili limedhihirishwa na Waziri wa Tamiseni.
Ofisi za serikali hasa za huko halimashauri kumegeuka madanguro kati ya wakurugenzi na watumishi wa kike.
DED na DC, DAS (Viongozi wa chini ya TAMISEMI) hawaruhusiwi kusafiri na wafanyakazi wao eti kwasababu ya kwenda kufanya Kazi.Ukiwa Na mchumba una malengo naye akikuambia nafanya kazi kwa DED ni bora kuanza kutafuta msichana Mwingine Safari haziishi mara naenda kwenye kikao nje ya halmashaur juwa anaenda kwenye kazi maalumu
Na hao ndio wake zao.Liverpool VPN katoka kusema hapa juzi juzi tu
Kwani wakiwa wamama ndo watakua hawaliwi na vijana? Kuna wakuu wa idara kibao hapa wanapelekewa moto na mayankiDawa ndogo tu, ma DED wote wawe akina Mama na akina dada.
Kwani Chadema siyo wazinzi??! Hivi mwenyekiti wenu (terrorist suspect) amezalisha wangapi hapo Ufipa??!!Ccm ni wazinzi na waasherati
CCM kumejaa madela na madela yamejaa kwa mamaKimbo Buza. Tatizo la nyumba moja halifanani na nchi nzima.Kwani Chadema siyo wazinzi??! Hivi mwenyekiti wenu (terrorist suspect) amezalisha wangapi hapo Ufipa??!!
Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
Acha kuchanganya mada, tangu lini kuzalisha ikawa haramu? Huna uwezo wa kubishana na Mimi hata hivyo!Kwani Chadema siyo wazinzi??! Hivi mwenyekiti wenu (terrorist suspect) amezalisha wangapi hapo Ufipa??!!
Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ummy Mwalimu, amedai kuwa amebaini kuwapo wakurugenzi wanaume kutumia vyeo kujihusisha kimapenzi na watumishi wa kike.
Amesema tabia ya wakurugenzi hao inasababisha baadhi ya watumioshi kupigana kwa sababu yao.![]()