Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Amesema “Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kusimama imara katika kuongoza mapambano dhidi ya #CoronaVirus hadi sasa ambapo Ugonjwa huo unaelekea kuisha nchini Tanzania”
Ameeleza kuwa “Katika Mikoa hiyo, upo Mkoa wa Dodoma na nyie ni mashahidi kama mlivyoona katika Kituo chetu cha Afya cha Mkonze. Ndiyo maana nimepita sijavaa mask (barakoa) kwasababu zaidi ya wiki hakuna Mgonjwa wa #Corona”
“Nitumie fursa hii kuwapongeza watoa huduma za Afya. Majemedari na makamanda wetu tunawapongeza kwa kazi nzuri na kubwa mliyofanya katika kuwahudumia Wagonjwa lakini mmeniambia na nyie hapa hakuna aliyepata maambukizi.”
Hata hivyo amewaomba Watanzania wasibweteke na waendelee kuchukua tahadhari kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Wataalamu wa Afya ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara na kuhakikisha wanavaa barakoa wakiwa katika mikusanyiko