Waziri Ummy: Mikoa zaidi ya 15 haina mgonjwa yeyote wa Corona

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756

Amesema “Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kusimama imara katika kuongoza mapambano dhidi ya #CoronaVirus hadi sasa ambapo Ugonjwa huo unaelekea kuisha nchini Tanzania”

Ameeleza kuwa “Katika Mikoa hiyo, upo Mkoa wa Dodoma na nyie ni mashahidi kama mlivyoona katika Kituo chetu cha Afya cha Mkonze. Ndiyo maana nimepita sijavaa mask (barakoa) kwasababu zaidi ya wiki hakuna Mgonjwa wa #Corona”

“Nitumie fursa hii kuwapongeza watoa huduma za Afya. Majemedari na makamanda wetu tunawapongeza kwa kazi nzuri na kubwa mliyofanya katika kuwahudumia Wagonjwa lakini mmeniambia na nyie hapa hakuna aliyepata maambukizi.”

Hata hivyo amewaomba Watanzania wasibweteke na waendelee kuchukua tahadhari kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Wataalamu wa Afya ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara na kuhakikisha wanavaa barakoa wakiwa katika mikusanyiko
 
Kwa mujibu wa mh Ummy Mwalimu, mikoa 15 haina corona kabisa! Dodoma ni mkoa mmojawapo! Nadhani wale wagonjwa wanne wanazunguka sana lakini hawajafika kwenye mikoa 15! Hongeraa!
 
Hao wagonjwa wanne (4) waliokuwa wamebaki hakuna aliyepona kati yao? Au wapo ICU?
 
 
Na wale madereva 198 waliorudishwa kutoka Kenya wakiwa Positive? Wamepona? Au?
Haijulikani, inamaana Kenya, Uganda, Rwanda, Zambia wote wameungana na mabeberu kupambana na sisi, kuathiri sekta yetu ya utalii na Burundi tu ndio jirani mwema 😀
 
mikoa zaidi ya 15. mbona sentensi imeacha mwanya wa kuweka namba yoyote mtu anayotaka. mfano gazeti likiandika mikoa 25 haina corona itakua bado ni sahihi kwa mujibu wa waziri wa afya
 
Taarifa yako tumeipokea Ila angalia yasitokee yanayoendelea huko burundi.eleza ukweli wa covid 19.tusije kuumbuka baadaye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…