Waziri Ummy Mwalimu kupunguza idadi ya idara ndani ya Halmashauri nchini ili kupunguza matumizi na kuongeza ufanisi

mimi napendekeza badala ya kuunganisha idara za Elimu ( msingi na sekondari) iwe moja, sekondari zingerudishwa kule ziliko kuwa Wizara ya Elimu...huku ziliko zimeshushwa hadhi sekondari zimekuwa kama shule za msingi tangu uendeshwaji wake hadi hadi watu wake hawajiamini...ma DEO wamekuwa kama miungu watu
 
Kuna changamoto kubwa kwenye kuunganisha idara.
Km lengo kupunguza matumizi tungeanza na idadi ya mawaziri,posho za wabunge na mshahara yao yaani staili zao na halmashauri km vipi idara zifutwe kila kitengo kijitegemee ili kupata uwezo uwajibikaji na ufanisi na kupunguza matumizi unless otherwise mkuu wa idara ni mratibu km lengo ni ufanisi basi mfano fedha na mipango fedha isiwe idara na mipango isiwe kitengo bali vyote viwili viwe vitengo na mkuu wa idara ababe jina la idara.na anaweza toka fedha au mipango .
Ufanisi ndani ya Halmashauri imekuwa zero na bila Halmashauri hakuna serikali kuu. Kwa maana hiyo wakuu wa idara ndani ya Halmashauri wanaotakiwa wafanyiwe interview na vetting ya hali ya juu ili kupata watendaji walio tukuka na wenye kasi ya hali ya juu ya utendaji. Uteuzi wa wakuu wa idara una ukakasi mkubwa ulioambatana na Rushwa. Ukuu wa idara umekuwa unanunuliwa kwa fedha. Au kupewa kama fadhila .
 
Km suala ni vetting na upatikanaji wake basi ni tatizo la mifumo yetu.
Changamoto ni kuziondoa baadhi ya idara au kuziunga na zile ambazo hazina ukaribu wa kiutendaji zaidi ya kisera.
 
MKUU wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ameamuru watumishi walioiba zaidi ya shilingi milioni 867 wawe wamezirudisha ifi kapo Juni 30, mwaka huu.

Fedha hizo zinazodaiwa kuibwa kwenye halmashauri tano, zinakadiriwa kuweza kugharamia ujenzi wa vituo viwili vya afya. Mrindoko alitoa agizo hilo ofisini kwake wakati akiwakaribisha wakuu wa wilaya za Mlele, Mpanda na Tanganyika waliohamishiwa mkoani humo.

Alisema amefanya ziara katika halmashauri tano za mkoa huo ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Halmashauri ya Manispaa Mpanda, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Nsimbo iliyopo katika Wilaya ya Mpanda na kubaini ubadhirifu wa fedha za serikali.

Kwa mujibu wa Mrindoko, alibaini hakuna halmashauri hata moja isiyo na ubadhirifu katika mapato yanayokusanywa katika vituo vya ushuru na kuingizwa kwenye akaunti za halmashauri.

Alisema katika baadhi ya halmashauri, fedha nyingi zilitumika nje ya mifumo ya serikali au zimepotea au hazikuingizwa kwenye mfumo wa serikali.

Kaimu Katibu Tawala wa Serikali za Mitaa, Idara ya Serikali za Mitaa, Reginald Mhango, alisema baadhi ya watumishi katika Halmashauri za Mkoa wa Katavi, walipokea fedha kutoka kwenye vituo vya kukusanya ushuru kwa njia ya mfumo wa mapato, lakini hawakuziingiza kwenye mfumo wa ukusanyaji mapato wa serikali za mitaa (LGRCIS).

Mhango alisema Halmashauri ya Mlele imepokea na haijaingiza Sh milioni 457, Halmashauri ya Mpimbwe ilipokea na haijaingiza Sh milioni 52, Halmashauri ya Manispaa Mpanda Sh milioni 138, Halmashauri ya Nsimbo Sh milioni 71 na Halmashauri ya Tanganyika zaidi ya Sh milioni 149.

Mrindoko aliagiza fedha hizo zitafutwe kokote zilipo na ziingizwe kwenye akaunti za serikali ili ziweze kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.
 
Someni hapa
 
Mh. Waziri Ummy Mwalimu. Pamoja na jitihada zako za kupambana na tamisemi, ni vema sasa ukapunguza idadi ya idara zilizopo ndani ya Halmashauri na kuongeza vitengo zaidi ilu kupunguza matumizi na kuongeza utendaji. Mfano, kuunganisha idara ya elimu msingi na elimu secondary kuwa idàra moja ya Elimu.

Pili maendeleo ya jamii na afya kuwa idàra moja Ila maendeleo ya jamii iwe kitengo. Idara ya mipango na fedha kuwa moja. Idara ya mipango kuwa kitengo. Pia ukumbuke wakuu wa idara hulipwa mishahara mikubwa bila ufanisi wowote.
Nafikir ili kuongeza ufanisi wakuu wa idara na vitengo wangekuwa wanapewa mikataba ya miaka mitatu asipo perform hakuna kurenew, anaachia ngazi.
 
Mfano kuna halmshauri ziko mjini hakuna nyuki Wala misitu unakuta kuna mkuu wa idara au kitendo Cha nyuki na misitu.
Hehehehehee....hihihihihihi.....Mbavu zangu; Mkuu unasema uongo hakuna kitu kama hicho; thibitisha!
 
Kwanini hazifai kuunganisha?
Zinaweza kabisa kuunganishwa. Kwa mfano, wizarani kuna Katibu mkuu mmoja tu, wengine ni ama manaibu katibu mkuu au wakuu/ wakurugenzi wa vitengo ama vya sekondari, msingi, elimu ya juu, vyuo, nk. na kazi inaendelea.
 
Back
Top Bottom