Waziri Ummy Mwalimu kwa hili la makato ya miamala jitafakari, hautoshi tena

Waziri Ummy Mwalimu kwa hili la makato ya miamala jitafakari, hautoshi tena

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Nimemsikiliza kwa makini sana Waziri Ummy Mwalimu akipigia chapuo makato ya miamala na kusema tutaenda kujenga shule, mara barabara za vijijini mara sijui hospitali.

Ummy ameyazungumza haya saa chache tu kabla ya Raisi Mama Samia kuingilia Kati.

Hivyo sasa hivi Waziri Ummy atabadili tena gia angani na kuanza kusema haya makato hayafai.

Hawa ndio viongozi wa Serikali, Leo wanakuaminisha hivi kesho boss wao akibadilika nao wanabadilika.

Serikali umeonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye hili.

Rais pia asiwe anasaini bila kujiridhisha , hii sio Mara ya kwanza kwa Mama Samia kukosea kwa aina hii. Inaanza kuleta mashaka na wasiwasi kuwa huenda akawa anasaini vitu ambavyo hata yeye havijui.

Sikubaliani na wanaosema sijui Mwigulu anamuangusha, kwanini amuangushe ikiwa yeye ndio boss na ndio alimteua?

Hivyo kwangu naona wa kuanza nae ni waziri Ummy kutokana na kauli zake.


20210719_125624.jpg
 
Kusema kweli Ummy alinichanganya mpaka mimi, coz mwanzo nilimsikia Rais akisema zile tozo zilikuwa ni kwa ajili ya kujenga barabara, sasa ghafla Ummy nae akaja na suala la kujenga madarasa, hii mambo ya kupigana tafu ili kujibu yasiyohusu wizara yake itamuharibia, aache kila waziri ajibu maswali ya wizara yake.
 
Kusema kweli Ummy alinichanganya mpaka mimi, coz mwanzo nilimsikia Rais akisema zile tozo zilikuwa ni kwa ajili ya kujenga barabara, sasa ghafla Ummy nae akaja na suala la kujenga madarasa, hii mambo ya kupigana tafu ili kujibu yasiyohusu wizara yake itamuharibia, aache kila waziri ajibu maswali ya wizara yake.
Hamna kitu humo
 
Ummy sidhani kama ana quality ya kuwa alipo

Sent using Jamii Forums mobile app
Tukiachana na tozo, Ummy anabebwa, hana uwezo kupewa wizara labda idara fulani tu. Nchi hii kuna watu wanabebwa sana na wenye uwezo wanawekwa kando.

Kuhusu tozo siwezi kumlaumu kwani bajeti ikishapitishwa lazima kila waziri aitetee, huwezi kwenda kinyume na hili labda uamua kuachia ngazi.
 
Tukiachana na tozo, Ummy anabebwa, hana uwezo kupewa wizara labda idara flani tu.
Nchi hii kuna watu wanabebwa sana na wenye uwezo wanawekwa kando.

Kuhusu tozo siwezi kumlaumu kwani bajeti ikishapitishwa lazima kilavwaziri aitetee, huwezi kwenda kinyume na hili labda uamua kuachia ngazi.
Kwani wote walibwabwaja? Mbona wengine walikaa kimya? Au kihelehele cha kutaka kusikika?
 
Hawa wanasiasa wapo radhi kuhongwa na mabenk yaliyoshindwa ushindani Ili kuhalalisha ujambazi wao
 
Hii nchi ukiwa mkweli unaonekana adui, angalie kwa SAG wetu walivyomfanyia, hivyo kina ummy bora waendelee kusifu na kuabudu tu, ndo walivyo kalilishwa
 
Maoni ya Waziri ni sahihi,hii nchi tukiendelea kuleana hatuwezi kutoka hapa na ulalamishi ndio jadi ya watu wa nchi hii.

Rais kaniudhi Sana hatuwezi kuwa na uongozi usio na msimamo, Vijijini huko Hali za maisha ni mbaya
 
Back
Top Bottom