Waziri Ummy Mwalimu kwa hili la makato ya miamala jitafakari, hautoshi tena

Waziri Ummy Mwalimu kwa hili la makato ya miamala jitafakari, hautoshi tena

Nimemsikiliza kwa makini sana Waziri Ummy Mwalimu akipigia chapuo makato ya miamala na kusema tutaenda kujenga shule, mara barabara za vijijini mara sijui hospitali.

Ummy ameyazungumza haya saa chache tu kabla ya Raisi Mama Samia kuingilia Kati.

Hivyo sasa hivi Waziri Ummy atabadili tena gia angani na kuanza kusema haya makato hayafai.

Hawa ndio viongozi wa Serikali, Leo wanakuaminisha hivi kesho boss wao akibadilika nao wanabadilika.

Serikali umeonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye hili.

Rais pia asiwe anasaini bila kujiridhisha , hii sio Mara ya kwanza kwa Mama Samia kukosea kwa aina hii. Inaanza kuleta mashaka na wasiwasi kuwa huenda akawa anasaini vitu ambavyo hata yeye havijui.

Sikubaliani na wanaosema sijui Mwigulu anamuangusha, kwanini amuangushe ikiwa yeye ndio boss na ndio alimteua?

Hivyo kwangu naona wa kuanza nae ni waziri Ummy kutokana na kauli zake.

View attachment 1859540
Hii inaonyesha udhaifu mkubwa katika administrative machinery yetu pamoja na bunge.
 
Back
Top Bottom