Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Leo, Waziri Ummy Mwalimu amesema Maduka yote ya dawa nje ya hospitali yanatakiwa kuwa umbali wa mita 500. Amesema Sheria hii aliipitisha yeye kabla sijaondoka Wizarani na kuongeza kuwa Maduka yaliyo ndani ya Mita 500 ndani ya Hospitali Nchi nzima wanakwenda kuyaondo.
Waziri Ummy amehoji: "Hospitali dawa hakuna, kwanini maduka ya nje dawa zipo? Haikubaliki"
NUKUU
“Ninatuma salamu maduka yote ya dawa lazima yawe mita 500 kutoka ndani ya hospitali, tunakwenda kuyaondoa ifikapo Julai Mosi mwaka huu tulishatoa muda wa kutosha kufikia Juni 30 yawe yameondoka.
“Wamiliki wanafanya kinyume cha sheria nipo na mfamasia Mkuu wa serikali hapa, tulitunga na tulipitisha kanuni maduka yote yawe mita 500 kutoka hospitalini nikaambiwa waziri kuna wengine walipewa leseni kabla, hivyo tumebakisha miezi mitano hakuna cha msalie mtume wala kuomba radhi,”
''Mwananchi anakosaje dawa? Suala hili ni la pande mbili MSD na hospitali na nilishatoa maagizo. Uwepo wa haya maduka yanachangia udokozi wa dawa na yanaondoa imani kwa wananchi kwamba angalau kuna usimamizi mzuri wa dawa vituoni,”
Pia soma

- Mnaopinga uondoaji wa maduka ya dawa maeneo ya hospitali mnaujua ukweli? (Nov 14, 2015)
- Maduka ya Dawa yaliyo nje ya mageti ya Hospitali za Serikali huwa na dawa muda wote lakini ndani ya Hospitali husika hamna dawa (Jan 11, 2022)
- Maduka yote ya dawa nje ya hospitali za Serikali marufuku (Nov 13, 2015)