Waziri Ummy Mwalimu: Maduka ya Dawa nje ya hospitali yaliyo ndani ya mita 500 kuondolewa

Waziri Ummy Mwalimu: Maduka ya Dawa nje ya hospitali yaliyo ndani ya mita 500 kuondolewa

Asante Waziri kwa jitihada zako za kuhakikisha sekta ya afya inawajibika ipasavyo kwa wananchi.

Lakini naona kama unazunguka sana kuhusu kutatua tatizo la uhaba wa dawa mahospitalini.

Wiki iliyopita hapa JF tulitoa maelezo kwa kifupi kuhusu sababu za uhaba wa dawa kwamba ni kwasababu ya Uongozi mbovu wa MSD.

Achana na kukimbizana na hayo maduka ya dawa yaliyokaribu na hospitali maana haitakusaidia kitu kwanza dawa zenyewe hakuna. Fuatilia kilichoandikwa humu JF na ndo mwarobaini wenyewe.


Halafu inaonekana kama vile vionvozi wa hii Serikali mnaogopa kuuwajibisha uongozi wa MSD, mmekuwa mkiyalea matatizo pale Bohari ya Dawa tangu wakati wa Dorothy. Leo tena nimemsikia PM Majaliwa akiwa Manyara akiibembeleza MSD kuhusu kupeleka dawa Manyara, hivi MSD wanatakiwa wafanye kazi kama zimamoto kila wakati wakati hiyo ndo kazi yako?

Pelekeni nguvu zote MSD ili dawa zinunuliwe maana Serikali ya Mama Samia ilishaleta hela kibao hapa MSD.
 
Fikiria vizuri hapo Mhe Waziri! Kuna wakati Hospitali za Serikali hukosa dawa kwasababu ya kukosa fedha au wanapoenda MSD hukosa dawa husika. Maduka mengine ya watu binafsi huwa wanaagiza dawa kutoka sehemu mbalimbali. Hata Kama Kuna watumishi wasio waaminifu ambao huiba dawa na kuziuza kwa maduka hayo, ni kitu gani kitazuia wasiuze au kuiba dawa wakati maduka ya watu binafsi yakiwa mbali na Hospitali?
Pia tukumbuke kwamba maduka haya ya nje ya hospital Mara nyingi huwa mkombozi kwa wagonjwa pindi dawa zinapokosekana wodini, ambapo ndugu hutumwa kwenda kununua dawa husika bila kuchelewa.
Serikali iwadhibiti watumishi wake wasiibe kama ni kweli wanaiba,Ihakikishe uwepo wa dawa Aina zote katika vituo vyake vya kutolea huduma,jambo ambalo ni gumu Sana,Kwa sababu daktari huandika dawa Kwa mtazamo wake na sio kuangalia kilichopo pharmacy ya Kituo.
Mwizi wa hizo dawa anaweza kuiba mkoa X na kwenda kuuza mkoa y.Hivyo Hilo tamko na hiyo Sheria kama Ipo haina tija.Ni maamuzi ya kihisia zaidi.
 
Wizara imepata chiriku, Kila wiki ni matamko na makatazo na mikwara ya kufa mtu,

Huyu mmama anapenda kuongea ongea sana, kila analoliwaza yeye anataka aliongee
Na kwanini hyo maduka yabanane kaibu na hospitali? Waziri yuko sahihi sana, Ummy ni miongoni mwa mawaziri jembe nchi hakuna asiyemfahamu. We inaonekana umeguswa. Hamna hata ubinadamu mnavizia kuwaibia wagonjwa wakati na nyie ni wagonjwa watarajiwa. Oneni hata aibu.
 
Yaani sababu hasa ni nini?..weka na sababu, mfano mimi nina frame zimepakana na hospitali na wamefungua pharmacy, sasa watakuja kuondoa hiyo pharmacy na kodi nani atamrudishia?
ndiyo sheria imeshatungwa utajuana na mwenye nyumba. Kutokujua sheria haikuoatii udhuru.
 
Yaani mambo haya ya kutaka serikali kujaribu ku' micromanage' everything, hata maisha ya watu na waendelee kutaabika kutokana na serikali yenyewe, kutowajibika kuhakikisha hospitali zina dawa za kutosha, sasa wananchi wafanyeje baada ya kukosa dawa hospitalini?? Kama dawa zingekuwa zapatiksns hospitalini, sidhani kama kuna mtu angelazimika kufuatia nje kwenye maduka hayo...Kaazi kwelikweli....

M
Km hujaelewa sidhani km utakuja kuelewa. Umeambiwa watumishi wa Hospitali wasio waaminifu wanakula njama na wenye maduka ya dawa kwa kuuziwa madawa ya serikali na ndio sababu mojawapo inayofanya hospitali nyingi za serikali kuishiwa dawa mapema.
 
Leo, Waziri Ummy Mwalimu amesema Maduka yote ya dawa nje ya hospitali yanatakiwa kuwa umbali wa mita 500. Amesema Sheria hii aliipitisha yeye kabla sijaondoka Wizarani na kuongeza kuwa Maduka yaliyo ndani ya Mita 500 ndani ya Hospitali Nchi nzima wanakwenda kuyaondo.

Waziri Ummy amehoji: "Hospitali dawa hakuna, kwanini maduka ya nje dawa zipo? Haikubaliki"

NUKUU
“Ninatuma salamu maduka yote ya dawa lazima yawe mita 500 kutoka ndani ya hospitali, tunakwenda kuyaondoa ifikapo Julai Mosi mwaka huu tulishatoa muda wa kutosha kufikia Juni 30 yawe yameondoka.

“Wamiliki wanafanya kinyume cha sheria nipo na mfamasia Mkuu wa serikali hapa, tulitunga na tulipitisha kanuni maduka yote yawe mita 500 kutoka hospitalini nikaambiwa waziri kuna wengine walipewa leseni kabla, hivyo tumebakisha miezi mitano hakuna cha msalie mtume wala kuomba radhi,”

''Mwananchi anakosaje dawa? Suala hili ni la pande mbili MSD na hospitali na nilishatoa maagizo. Uwepo wa haya maduka yanachangia udokozi wa dawa na yanaondoa imani kwa wananchi kwamba angalau kuna usimamizi mzuri wa dawa vituoni,”


Pia soma

View attachment 2094049
Pale akili ndogo zinapotawala akili kubwa...Aisee...sijaelewa lengo la huyu Mama eti waziri ni lipi hapa? Kwani wakipeleka hata mita 1,000 dawa zitapatikana Hospitali au itakuwa ndio mbaya zaidi kwa wagonjwa kutembea hayo makilomita kutafuta dawa? mwizi ni mwizi tu na dawa yake ni kumzuia asiibe na sio vinginevyo..
 
Simple logic wao wameshindwa nini kuhakikisha dawa zinapatikana hospitali muda wote ili watu wasiende maduka ya nje?

That's hasty generalization.
 
Na kwanini hyo maduka yabanane kaibu na hospitali? Waziri yuko sahihi sana, Ummy ni miongoni mwa mawaziri jembe nchi hakuna asiyemfahamu. We inaonekana umeguswa. Hamna hata ubinadamu mnavizia kuwaibia wagonjwa wakati na nyie ni wagonjwa watarajiwa. Oneni hata aibu.
Karibu na hosp ndio wateja wao walipo ni sawa na uulize mbona stand za mabasi kuna vyoo vya kulipia
 
Yakae mita 510 tuone anatatua nini! Je, waziri anamaanisha kwamba duka binafsi la dawa likiwa umbali wa viwanja vitano vya mpira, ndio dawa zitapatikana hospitali?!!

Zipo zahanati hazipo karibu na duka lolote binafsi la dawa huko Bukombe, na bado hazina dawa. Hizi shida ni nini?

Waziri analenga kutatua tatizo gani? Au upeo wa kutatua matatizo yetu umfikia kikomo!!
Anaongea ili mradi tu naye aonekane ameongea .naona amepanic yeye amepeleka kiasi gani msd

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kauli ya ovyo kabisa nimewahi kuisikia nchi yenyewe maskini kule hospitali dawa hawana bima zenyewe mpaka mtu awe kaajiriwa, pale temeke operation mdogo laki 5, muhimbili kule ndio kabisa leo uzuie maduka ya dawa mita 500 kutoka hospitali kwa lipi kubwa.,

Ni vile kiongozi akiwa kwenye madaraka anaona hali yake anavyoishi na familia yake ndivyo watu wengine wanaishi., Kama mumeboresha mahospitali kiasi basi hao wenye maduka wataondoa maduka yao automatically watakosa wateja mana hospitali kuna kila kitu
Yeye anajali nini bana mshahar 11m posho ya mafuta umeme bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahahahaha yakiwa ndani ya mita 500 inaonekana maduka binafsi yanatumia magnetic-field kuhamisha madawa toka msd ya hospitali za serikali hivyo wagonjwa hukosa dawa, ngoja tuone yakiwa zaidi ya hizo mita labda dawa zitakwepo watu hatutaambiwa hakuna dawa kanunue
Mahitaji ya hospital ni makubwa mno sasa wanaletewa vimilioni viwili ndo wanakuja kusingizia wizi wa dawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena uwe na moyo wa chuma haswa, Mimi huwa nawavulia kofia watu waliofanikiwa kibiashara bongo hii na najifunza vingi kutoka kwao.

Serikali na taasisizake na mamlaka zake zote zipo kwa ajili ya makatazo, mazuio, ukamataji, ukusanyaji, ufungiaji, bila kujali mfanyabiashara huyu anabaki na nini na anasaidiwa na nani ikiwa kila mtu yupo kwa ajili ya uharibifu.
Halafu wanategemea na kodi ije kuwalipia mafuta ya v8 na allowance kibao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom