Waziri Ummy Mwalimu: Maduka ya Dawa nje ya hospitali yaliyo ndani ya mita 500 kuondolewa

Waziri Ummy Mwalimu: Maduka ya Dawa nje ya hospitali yaliyo ndani ya mita 500 kuondolewa

Wataalamu wanaoweza kuingia hospitali jamaa wakisema dawa hakuna na kufanya tracing ya papo kwa papo kwa kuchukua prescription tu ya mgonjwa na kubaini uongo wao amuwataki.

Mnachezea sana maisha ya watu. It is never personal simjui Ummy Mwalimu wala sina chuki nae binafsi. Ila hiyo wizara ni too technical for her.

Waingereza wana msemo it’s only easier if you know it, tatizo wengi awakumuelewa Dr Gwajima kwa sababu ya limitations zao ya management za afya.

Kwenye hiyo video if you know anything about auditing anachoongea ni kwamba anaijua inventory system ya dawa. Kuanzia kuagiza, idadi inayokuja na zinazotoka packet to packet akiamua kufanya full audit; na kawapa mfano live.

Akikuta zimepungua anaweza kukwambia kiasi gani kimedokolewa. Kwa sababu anaijua inventory system yote.

Utaki kujua amegundua vipi damu azija pelekwa maabara for that inabidi uwe muelewa wa quality management ya afya na madhara yake kwa watumia huduma unapochelewesha vipimo.

Majungu mengine ya siasa yana madhara sana kwa raia wanaotumia hizo huduma.

Inawezekana Tanzania kuna wataalamu wengi lakini binafsi nilio wasikia wenye viwango vya kimataifa namkubali Dr Kimei kwenye banking na Dr Gwajima kwenye health management she is something else basi tu anaishi nchi ya ovyo.

Dr Gwajima ata ulaya anapata senior management post kwenye University Hospital (ni hospitali kubwa na za kimataifa) ana sifa zote.

Kuna maamuzi yana madhara wahusika awaelewi tu. Kusema Ummy Mwalimu ni bora kushinda Dr Gwajima wizara ya afya ni kujifurahisha, but in the process kuna costs za maisha ya watu.
 
Kusumbua tuu ndug wa wangonjwa hosptali zetu za uma hazina hata graves mtu afata mail 1 huko wakati mgonjwa ana vuja damu tutakufa wengi
 
Watekeleza haya matamko sasa ni muda wa kutumia akili zao,sio kila tamko ni la kulifanyia kazi,sjui kama waziri hata hzo mita 500 anajua umbali wake
 
Turundikane maduka ya MSD??
Lengo kuua wagonjwa au kuokoa maisha ya wagonjwa??

Au lengo ni nini?? Na Kwa Sheria ipi??

Ummy alikuwa ana akili nafikiri kwenda TAMISEMI amerudi akili ka zimemixiwa za mtendaji, mwenyekiti serikali ya mtaa, mjumbe, mwalimu wa darasa la kwanza, mwalimu mkuu msaidizi e.t.c

Ummy aache ulimbukeni, ameanza kukera jamii na na matamko yake, yasiyo na mbele wala nyuma! Yana hang Tu!
 
Wataalamu wanaoweza kuingia hospitali jamaa wakisema dawa hakuna na kufanya tracing ya papo kwa papo na kubaini uongo wao amuwataki.

Mnachezea sana maisha ya watu. It is never personal simjui Ummy Mwalimu wala sina chuki nae binafsi. Ila hiyo wizara ni technical.

Waingereza wana msemo it’s only easier if you know it, tatizo wengi awakumuelewa Dr Gwajima.

Kwenye hiyo video if you know anything about auditing anachoongea ni kwamba anaijua inventory system ya dawa. Kuanzia kuagiza, idadi inayokuja na matumizi packet to packet.

Akikuta zimepungua anaweza kukwambia kiasi gani kimedokolewa. Kwa sababu anaijua inventory system akipata prescription tu.

Utaki kujua amegundua vipi damu azija pelekwa maabara for that inabidi quality management ya afya.

Majungu mengine ya siasa yana madhara sana kwa raia wanaotumia hizo huduma.

Inawezekana Tanzania kuna wataalamu wengi lakini katika nilio wasikia wenye viwango vya kimataifa binafsi namkubali Dr Kimei kwenye banking na Dr Gwajima kwenye health management she is something else basi tu anaishi nchi ya ovyo.

Dr Gwajima ata ulaya anapata senior management post kwenye University Hospital (ni hospitali za kubwa na za kimataifa) ana sifa zote.

Kuna maamuzi yana madhara wahusika awaelewi tu. Kusema Ummy Mwalimu ni bora kushinda Dr Gwajima wizara ya afya ni kujifurahisha, but kuna costs za maisha ya watu.

Kuna wizara inabisi wawe wanapewa watu wenye taaluma inayoendana na field husika
 
Leo, Waziri Ummy Mwalimu amesema Maduka yote ya dawa nje ya hospitali yanatakiwa kuwa umbali wa mita 500. Amesema Sheria hii aliipitisha yeye kabla sijaondoka Wizarani na kuongeza kuwa Maduka yaliyo ndani ya Mita 500 ndani ya Hospitali Nchi nzima wanakwenda kuyaondo.

Waziri Ummy amehoji: "Hospitali dawa hakuna, kwanini maduka ya nje dawa zipo? Haikubaliki"

NUKUU
“Ninatuma salamu maduka yote ya dawa lazima yawe mita 500 kutoka ndani ya hospitali, tunakwenda kuyaondoa ifikapo Julai Mosi mwaka huu tulishatoa muda wa kutosha kufikia Juni 30 yawe yameondoka.

“Wamiliki wanafanya kinyume cha sheria nipo na mfamasia Mkuu wa serikali hapa, tulitunga na tulipitisha kanuni maduka yote yawe mita 500 kutoka hospitalini nikaambiwa waziri kuna wengine walipewa leseni kabla, hivyo tumebakisha miezi mitano hakuna cha msalie mtume wala kuomba radhi,”

''Mwananchi anakosaje dawa? Suala hili ni la pande mbili MSD na hospitali na nilishatoa maagizo. Uwepo wa haya maduka yanachangia udokozi wa dawa na yanaondoa imani kwa wananchi kwamba angalau kuna usimamizi mzuri wa dawa vituoni,”

Pia soma

View attachment 2094049
1. Nionavyo mimi, hii siyo solution ya tatizo la ukosefu/upungufu wa dawa Muhimbili.
2. Kuna hospitali na karibu na hizo hospitali hakuna maduka ya dawa na still hospitali unakuta hakuna dawa.
3. Kama tatizo na kuuza dawa kwa wamiliki wa maduka ya dawa, solution yake ni kudhibiti huo uuzaji wa dawa.
4. Tatizo litakalojitokeza baada ya maduka ya dawa kuhama ni wagonjwa kwenda kununua dawa mbali tofauti na mwanzoni kwamba walikuwa na unafuu wa kununua dawa karibu.
5. Kama hao wenye maduka ya dawa ndio wanaonunua dawa hospitalini na kusababisha huo ukosefu/upungufu wa dawa kwa nini hawajachukuliwa hatua za kisheria?
6. Mimi nadhani kuna ukosefu/upungufu wa dawa na solution ingekuwa ni kuhakikisha dawa zinapatikana hospitalini na wagonjwa wanatibiwa kwa haraka iwezekanavyo, lakini agizo la waziri kwa maoni yangu yanalisukuma tatizo mbele zaidi.
 
Kuna wizara inabisi wawe wanapewa watu wenye taaluma inayoendana na field husika
Tatizo lenyewe ata wanapopewa huyo mtaalamu wengi awamtambui.

Wapiga majungu wengi ni watu ambao wao wenyewe kwa sasa wakiumwa wanaenda private.

Wasichojua ipo siku mirija itakata wakiwa wazee wanaenda kukumbana na hizo hadaa za huduma mbovu.
 
Hamna haja ya kuondoa yanasaidia sana mfano hospitali gloves hamna za kumzalishia mama MTU anenda nje chap chap ananunua kwenda nusu kilomita ni mbali mno

Sehemu zingine mawilayani miji midogo ukihesabu mita 500 toka hospitali ya serikali ilipo ni porini machakani kusikoishi watu kwenye majoka
Mkuu ni wewe🙄🙄
 
Watu wanataka aeleze mantiki na tija ya hiyo sheria. Inaendaje kuondoa tatizo. watu kama wewe ambao huwa hamjiulizi WHY ndio mnashangaa
Hata mm naona haitasaidia chochote Ila ndio najiuliza wabunge Wa Ccm walipokuwa wanapitisha hii Sheria waliwaza nn?
 
Leo, Waziri Ummy Mwalimu amesema Maduka yote ya dawa nje ya hospitali yanatakiwa kuwa umbali wa mita 500. Amesema Sheria hii aliipitisha yeye kabla sijaondoka Wizarani na kuongeza kuwa Maduka yaliyo ndani ya Mita 500 ndani ya Hospitali Nchi nzima wanakwenda kuyaondo.

Waziri Ummy amehoji: "Hospitali dawa hakuna, kwanini maduka ya nje dawa zipo? Haikubaliki"

NUKUU
“Ninatuma salamu maduka yote ya dawa lazima yawe mita 500 kutoka ndani ya hospitali, tunakwenda kuyaondoa ifikapo Julai Mosi mwaka huu tulishatoa muda wa kutosha kufikia Juni 30 yawe yameondoka.

“Wamiliki wanafanya kinyume cha sheria nipo na mfamasia Mkuu wa serikali hapa, tulitunga na tulipitisha kanuni maduka yote yawe mita 500 kutoka hospitalini nikaambiwa waziri kuna wengine walipewa leseni kabla, hivyo tumebakisha miezi mitano hakuna cha msalie mtume wala kuomba radhi,”

''Mwananchi anakosaje dawa? Suala hili ni la pande mbili MSD na hospitali na nilishatoa maagizo. Uwepo wa haya maduka yanachangia udokozi wa dawa na yanaondoa imani kwa wananchi kwamba angalau kuna usimamizi mzuri wa dawa vituoni,”

Pia soma

View attachment 2094049
Narudia kusema na nitaendelea kusema; Nchi yetu tuna ombwe kubwa la Viongozi, na kama bado tunashindwa kutengeneza mikakati na mifumo ya kupata Viongozi Bora na wala si Bora viongozi au viongozi wa Mitandao, kwa kweli kama Taifa tunapotoka na ni hatari kwa mustakabili wa Taifa letu na kizazi kijacho.

Hivi kweli tatizo la kukosekana Madawa Hospitali ni sababu ya hayo maduka ya Dawa yaliyoko ndani ya mita 500 ktk Hospitali zetu? Je tunakwepa chanzo cha tatizo na kukimbilia na kusingizia maduka ya madawa binafsi yaliyo karibu na Hospitali? Je kwa upande wa wanao wauguza ndugu zao hapo hospitali, tunakuwa tunawasaidia au ndio tunawapa zaidi ugumu wa kuuguza ndugu zao na hata kuhatarisha maisha ya wagonjwa kwa kufanya hayo maduka yawe mbali zaidi na hospitali? Tumewafikiria wananchi hao wanaopigania maisha ya ndugu zao?

Kwa msingi mkuu wa Biashara yoyote ili ipate faida, kinachoangaliwa zaidi ni namba ya wateja na mahali. Sasa kwa duka la madawa, ni ukweli ulio wazi kuwa karibu na Hospitali ndio palipo na Biashara kubwa ya wateja wake. Na wametumia hiyo fursa baada ya kuona Hospitali za Serikali hazina dawa. Na wao wakaweka maduka pale yakiwa na Dawa zote zinazohitajika. Sio sahihi kuuliza kwanini Maduka binafsi yana dawa na hospitali hakuna Dawa, ni suala la utawala na usimamizi tu.

Ndio maana kwa miaka mingi, Taasisi nyingi zinazomilikiwa na Serikali zimeshindwa kufanya vizuri na nyingine kufa tofauti na taasisi binafsi ambazo zipo ktk sekta moja. Tatizo sio hayo yanayolalamikiwa, tatizo ni Usimamizi na uwajibikaji wa waliopewa mamlaka kusimamia masuala ya Uongozi ktk taasisi husika, tofauti na ktk taasisi na makampuni binafsi. Ni nadra sana kukuta hakuna dawa ktk hospitali za binafsi.

Mawazo yangu, tunahitaji kujitathmini sana Watanzania juu ya uwezo wa wenzetu waliopewa mamlaka kama wanatosha kweli, wao pia wajipime kama kweli wanafanya kile kilichokusudiwa kama viongozi.
 
Mkuu ni wewe🙄🙄
Ndio udhibiti ufanyike ndani ya hospitali sio kwenda kuparamia maduka ya watu nje waliyojiwekezea kwa mitaji mikubwa mikopo ya mabenki

Unashindwa kudhibiti mke au mime ndani unataka majirani wenye nyumba jirani na wewe wanaotembea na mmeo au mkeo wahame waende mbali nchi zingine!!! Hiyo sio solution mdhibitiane huko ndani

Udhaifu wa huko ndani msisukumie watu wengine wenye maduka nje
 
Wakikaa Karibu Wanaharibu nn? issue hapa Ni Dawa Kuwepo zote kwenye Hospitali za Serikali hilo tu basi...Mengine ni bla bla
 
wanapuyanga tu waache ayo maduka watanzania tununue dawa.
Kama ni wizi wa dawa unaanzia huko msd wakadhibiti huko.
 
Narudia kusema na nitaendelea kusema; Nchi yetu tuna ombwe kubwa la Viongozi, na kama bado tunashindwa kutengeneza mikakati na mifumo ya kupata Viongozi Bora na wala si Bora viongozi au viongozi wa Mitandao, kwa kweli kama Taifa tunapotoka na ni hatari kwa mustakabili wa Taifa letu na kizazi kijacho.

Hivi kweli tatizo la kukosekana Madawa Hospitali ni sababu ya hayo maduka ya Dawa yaliyoko ndani ya mita 500 ktk Hospitali zetu? Je tunakwepa chanzo cha tatizo na kukimbilia na kusingizia maduka ya madawa binafsi yaliyo karibu na Hospitali? Je kwa upande wa wanao wauguza ndugu zao hapo hospitali, tunakuwa tunawasaidia au ndio tunawapa zaidi ugumu wa kuuguza ndugu zao na hata kuhatarisha maisha ya wagonjwa kwa kufanya hayo maduka yawe mbali zaidi na hospitali? Tumewafikiria wananchi hao wanaopigania maisha ya ndugu zao?

Kwa msingi mkuu wa Biashara yoyote ili ipate faida, kinachoangaliwa zaidi ni namba ya wateja na mahali. Sasa kwa duka la madawa, ni ukweli ulio wazi kuwa karibu na Hospitali ndio palipo na Biashara kubwa ya wateja wake. Na wametumia hiyo fursa baada ya kuona Hospitali za Serikali hazina dawa. Na wao wakaweka maduka pale yakiwa na Dawa zote zinazohitajika. Sio sahihi kuuliza kwanini Maduka binafsi yana dawa na hospitali hakuna Dawa, ni suala la utawala na usimamizi tu.

Ndio maana kwa miaka mingi, Taasisi nyingi zinazomilikiwa na Serikali zimeshindwa kufanya vizuri na nyingine kufa tofauti na taasisi binafsi ambazo zipo ktk sekta moja. Tatizo sio hayo yanayolalamikiwa, tatizo ni Usimamizi na uwajibikaji wa waliopewa mamlaka kusimamia masuala ya Uongozi ktk taasisi husika, tofauti na ktk taasisi na makampuni binafsi. Ni nadra sana kukuta hakuna dawa ktk hospitali za binafsi.

Mawazo yangu, tunahitaji kujitathmini sana Watanzania juu ya uwezo wa wenzetu waliopewa mamlaka kama wanatosha kweli, wao pia wajipime kama kweli wanafanya kile kilichokusudiwa kama viongozi.
Hii haina tofauti na wale Polisi Dodoma waliosema kwamba wataanza kuyasindikiza mabasi ili yasiende spidi,yaani tunapenda solution za haraka ambazo hatuangalii hata kama zitakomesha tatizo na madhara yake ni yapi.
 
Wataalamu wa mita 500 nisaidieni duka LA dawa naweka wapi mfano ninalo muhimbili sasa nataka nilipeleke mita mia tano

Nashangaa Muhimbili mita mia tano za kwanza hata hazijatimia nakutana na hospitali ya serikali mnazi mmoja nao wanaha kutafuta mita mia tano toka hiyo hospitali waweke wapi sababu wametafuta mita mia tano hazijatimia wakakutana na Hospitali ya serikali ya Amana

Hivi kwa mita hizo mia Tano katikati ya jiji na Karikoo ina maana hakutakuwa na pharmacy hata moja ?

Uamuzi wa kijinga sanaf
 
Ila wadau hapa wabunge wa CCM ndio wakulaumiwa,akiwemo huyo Waziri mwenyewe,hili suala alilibua Majaliwa,Baadae Akapigilia msumari Mwendazake na sasa huyu kalikumbushia kwa kuwa muda wa kuyaondoa hayo maduka unaelekea mwishoni.

Hii nchi inahitaji mabadiliko makubwa sana,Na haya ndio madhara ya kutotaka mawazo mbadala huko bungeni.Hii tayari ni sheria wala sio tamko la Ummy tu.

Kama wanaona hii ndio muarobaini wa tatizo,Ngoja maduka yaondolewe tuone kama wizi wa dawa au ukosefu wa dawa utapungua.
 
Mita mia tano zitaondoa maduka yote ya dawa katikati ya jiji na yaliyoko kariakoo sababu yako karibu na hospitali za serikali za mnazi mmoja , hospitali ya Amana,Ocean Road na Muhimbili

Yote yako ndani ya mita mia tano
 
Waziri ni cheo kikubwa sana, Waziri ni kiongozi wa wizara anayezungukwa na kila aina ya resources zinazomuwezesha kufanya kazi zake kwa ufanisi....mpaka kutoa uamuzi maana yake watu wamefikiri na hapo ndio mwisho wamemaliza....
Na kama kufikiri kwenyewe ndo hivyo ina maana kuna tatizo kubwa kwa wanaomzunguka na yeye mwenyewe.
 
Leo, Waziri Ummy Mwalimu amesema Maduka yote ya dawa nje ya hospitali yanatakiwa kuwa umbali wa mita 500. Amesema Sheria hii aliipitisha yeye kabla sijaondoka Wizarani na kuongeza kuwa Maduka yaliyo ndani ya Mita 500 ndani ya Hospitali Nchi nzima wanakwenda kuyaondo.

Waziri Ummy amehoji: "Hospitali dawa hakuna, kwanini maduka ya nje dawa zipo? Haikubaliki"

NUKUU
“Ninatuma salamu maduka yote ya dawa lazima yawe mita 500 kutoka ndani ya hospitali, tunakwenda kuyaondoa ifikapo Julai Mosi mwaka huu tulishatoa muda wa kutosha kufikia Juni 30 yawe yameondoka.

“Wamiliki wanafanya kinyume cha sheria nipo na mfamasia Mkuu wa serikali hapa, tulitunga na tulipitisha kanuni maduka yote yawe mita 500 kutoka hospitalini nikaambiwa waziri kuna wengine walipewa leseni kabla, hivyo tumebakisha miezi mitano hakuna cha msalie mtume wala kuomba radhi,”

''Mwananchi anakosaje dawa? Suala hili ni la pande mbili MSD na hospitali na nilishatoa maagizo. Uwepo wa haya maduka yanachangia udokozi wa dawa na yanaondoa imani kwa wananchi kwamba angalau kuna usimamizi mzuri wa dawa vituoni,”

Pia soma

View attachment 2094049
Hii nchi ina vituko vya kujaza kitabu. Duka la dawa la hospitali halina dawa. Mgonjwa hajiwezi, halafu atoke jospitali atembee nita 500+kutafuta dawa duka binafsi. Ati duka likiwa karibu na hospitali kwanini liwe na dawa wakati la serikali halina?? Hii ni akili au matope?
Kwani kama dawa ni za wizi baada ya mita 500 wezi hawata weza kuzipeleka hapo??
 
Kwahiyo yakiwa nje umbali wa mita 500 ndio dawa zitakosekana kwenye hayo maduka? Au mimi kuna kitu sijaelewa?
Nahisi yakiwa umbali wa mita 500 dawa zitagoma kwenda huko. Hii itasaidia wagonjwa wazipate kwa urahisi hospitalini!

Hapa wafamasia na waziri wao wanazingua! Najua wanajua kuwa kwingineko mtu anafunga safari kwenda kuzitafuta dawa!

NB: Serikali ijiulize kwanini famasi zake zikose dawa zinazopatikana??
 
Back
Top Bottom