Waziri Ummy Mwalimu, waeleze wananchi kwamba ugonjwa uliogundulika Lindi ni rahisi zaidi kusambazwa na mbwa pia

Waziri Ummy Mwalimu, waeleze wananchi kwamba ugonjwa uliogundulika Lindi ni rahisi zaidi kusambazwa na mbwa pia

gimmy's

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2011
Posts
3,312
Reaction score
3,345
Salaam,

Hivi majuzi kulitokea taharuki ya ugonjwa uliosababisha sintofahamu kwa wakazi wa Lindi baada ya kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Dalili zilizoonekana kwa wagonjwa ilikua ni pamoja na homa kali,kuumwa viungo vya mwili pamoja na kutokwa na damu puani.

Mwanzoni ugonjwa huu haukuweza kufahamika lakini baada ya uchunguzi kufanyika leo waziri wa afya mh Ummy Mwalimu ameueleza uma kwamba hugonjwa huu unaitwa Leptopirosis.

Kwenye maelezo ya mh Ummy ameeleza kwamba asili ya ugonjwa huu ni kwa wanyama wa porini,lakini wanyama wa porini huweza kuwaambukiza pia wanyama wa majumbani kama paka na panya.

Kwangu kutokutajwa mbwa nimeona huwenda wananchi wakaacha kuchukua tahadhari kwa mbwa jambo ambalo ni hatari.

Ningependa kukazia kwamba kwa wale wanaofuga mbwa watakua wanafahamu kwamba ugonjwa huu ni common zaidi kwa mbwa kuliko hata paka.Mbwa huwa tunawachanja chanzo DHLPP.Hii chanjo huzuia magonjwa matano kwa wanyama na L ni kifupi cha leptopirosis.

Na ni kweli ugonjwa huu huweza kusambaa kutoka kwa wanyama walioathirika kuja kwa binadamu kwa kugusana na majimaji kama damu nk.

Nashauri mh Ummy kama wanaona tatizo hili ni kubwa ni vema wangechanja mifugo DHLPP hasa mbwa na paka kwani wanyama hawa wapo kwenye jamii hivyo huongeza uhatarishi wa maambukizi.

Asanteni.
 
Mama samia alikuwa sahihi sababu ingekuwa ajabu kiongozi mkubwa kuongea bila backup na kupangwa na wataalam.
Good to know.
 
Wewe umejuaje uhusika wa mbwa? Ni Mhehe?
Umeelewa Vibaya,issue ya msingi sio lazima mtu ale ndipo aambukizwe,ikitokea unajeraha lolote mwilini,majimaji kama mkojo ama damu yanaweza kukuambukiza hu ugonjwa.

Yeyote anaefuga mbwa hasa mbwa wakisasa huu sio ugonjwa mgeni kwenye masikio yake.

Ma Dr wa mifugo mara nyingi huwa wanaupata sana huu ugonjwa hasa wale wenye kutibu wanyama pasipo tahadhari kama kuvaa gloves.
 
Hakuna ugonjwa uitwao LECTOPIROSIS labda kama ulimaanisha leptospirosis
 
Ndo maana Mimi mazoea na paka na mbwa Sina kabisa.sio Kama nawachukia ila sipendi mazoea nao
 
Huo ugonjwa mbona kama siyo mpya? Huo ni Ebola ama Monkey fever. Kwann mnahangaika?
 
Hakuna ugonjwa uitwao LECTOPIROSIS labda kama ulimaanisha leptospirosis
Mimi ni raia wa kawaida,lengo langu lilikua kuokoa watanzania wenzangu na nashukuru wamenielewa,nimerekebisha,asante.
 
Back
Top Bottom