Waziri Ummy: Nakataza Michango Mashuleni, asiyekuwa na Sare za Shule acha asome

Huyu Mama afikiriwe nafasi za Juu hapo baadae,
 
Tujitafakari haya mambo eti tupo uchumi wa kati. Ukweli usemwe uzazi wa mpango kuwapotosha watu elimu bure, huduma afya zimeboreshwa mfyatuane!!!
 
Watoto wa ummy wanasoma international wenzao wanaambiwa msivae sare vaeni yeboyebo nchi hii bado tupo Karne 15
 
Ahsante,Waziri wetu,Ahsante Rais wetu kwa kuteletea Waziri,anayejuwa matatizo ya wananchi.
 
Mambo ya ajabu sana kwa kuharibu utaratibu uliowekwa. Mwanafunzi lazima aende akiwa ndani ya uniform.

Kuwaruhusu kwenda bila uniform ni presence mbaya sana, siku tutawaruhusu waingie darasani hata kama hawana daftari.
Ikiwa wewe una uwezo kumbuka wapo wasio na uwezo.Ikifika mwisho wa mwaka,kuna kulipia kodi ya pango la nyumba,watoto wakuwanunulia uniform sio mmoja,wapo wa ndugu na jamaa waliofiwa na wazazi wao.Sikukuu za mwisho wa mwaka.Wapo wenye wagonjwa,nk,wengine wanamsubiria michango ya ndugu na jamaa.
 
Wamepewa mda wajipange.
 
Hela za tozo zingenunua uniform,
Kwan madarasa yanajegwa kwa hela ya corona.
 
Binadamu Kila kitu kwake shida! Wangezuiliwa mngelaumu! Wameruhusiwa kwenda kwa muda bila uniform pia mnalaumu! Hakika duniani sio sehemu salama kwa watendao mema!!!
Umesema kweli tupu,watoto wengi wanashindwa kusoma kutokana na mahitaji ya shule,miongoni mwa hayo mahitaji ni sare za shule.Inasikitisha nilihudhuria kikao cha shule fulani,mtoto anavyaa sueta juu ya shati la shule siku zote,kumbe shati mgongoni ,mgongo wote uko wazi, limepasuka,walimu walipomuuliza,ndio akajieleza.
 
Ahsante Waziri,unajuwa matatizo ya unaowaongoza,Mungu akubariki sana.Rais wetu aliyekuteua wewe,alijuwa wazi uko vizuri.
 
Huo uhuru wakianza kuutumia vizuri ndipo itafahamika kama wamesaidia au wameharibu.
Walau uniform zinasaidia hususan upande wa nidham wanapokuwa nje ya viunga vya shule.
 
Sare ya shule huondoa matabaka shuleni, hapo moja kwa moja itaonekana asiye na sare ni maskini wa kutupwa.

Uniform si jambo la kupuuza.

Tunarudi enzi za mwalimu Nyerere.
 
Mambo ya ajabu sana kwa kuharibu utaratibu uliowekwa. Mwanafunzi lazima aende akiwa ndani ya uniform.

Kuwaruhusu kwenda bila uniform ni presence mbaya sana, siku tutawaruhusu waingie darasani hata kama hawana daftari.
Uwelewa mbaya,ukiangalia shule za private mwanafunzi anafika shuleni Hana uniform anaenda darasani mpaka itakapokuwa tayari Sasa ubaya upo wapi wa wazazi kupewa muda huku mtoto akiendelea na masomo?
Tuache kufikiria negative kila kijacho
 
Lengo la uniform ni mwanafunzi anapotoroka au akipata matatizo mtaani watu wanajua waanzie wapi; ni utambulisho wa mwanafunzi.

Ndio maana kwa wale waliosoma boarding ilikuwa tukitoroka shule kitu cha kwanza ni kuvua mashati yatakayo tutambulisha tumetoka shule gani au kutovaa uniform kabisa.

Huyu mama mweupe sijapata kuona halafu sijui kwanini wanapenda kumpa wizara kubwa na ngumu; it’s beyond me.
 
Kwahiyo watoto we unafikiria Kuna mtoto akidondoka kipindi hiki Cha likizo hawatasaidiwa kisa Hana uniform?
 
Nakumbuka form one headmaster alisema hatambui uniform nje ya shule lazima tutoe hela tupimishwe shuleni,tulitoa hela baadaye wanaume tumeletewa suruali nyeusi za mtumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…