Waziri Ummy: Nakataza Michango Mashuleni, asiyekuwa na Sare za Shule acha asome

Waziri Ummy: Nakataza Michango Mashuleni, asiyekuwa na Sare za Shule acha asome

Kwa speed hii ya Rais Samia, Tanzania huenda ikaibua mabilionea wapya 100 miaka miwili ijayo,Tufanye kazi kwa bidii zaidi
 
Uchumi wa kati hawawezi kugawa sare bure maana elimu tuliambiwa ni bure kuanzia awamu ya 5 na kwamba wasiotakiwa shule ni waliozaa tu
 
Hahahahhaahaa wanasema ogopa sana kuongozwa politicians.Huyu waziri ni Mwanasheria kwa taaluma yake lakini hajui umuhimu wa mwanafunzi kuwa ndani ya sare ya shule inamwepusha na mambo mengi including masuala ya kiusalama kwake.Hivi akibakwa itakuwaje?
Tunako elekea nusu ya shule wanafunzi watakuwa hawana Uniform
 
Hizi kauli mbona si mpya, tatizo liko wapi?.

Miezi kadhaa nyuma mapema asubuhi nilikutana na Kijana mdogo akiwa amevaa sare za shule ambazo zilikuwa zinasadifu tosha hali ya kiuchumi ya familia anayotokea.

Mtoto yule alikuwa anakwenda kama hataki huku usoni akionekana analia hivyo nikavutika kumuhoji kujua kulikoni...akasema Mama yake amempiga kwa sababu alikuwa anakataa kuondoka nyumbani bila kupewa mia tano ya mchango shuleni ambako nako akifika bila ya hiyo hela Mwalimu husika anamchapa.

Nilimpa mia tano na kumwambia akimbie awahi shuleni, walau akabadilika na kuonesha matumaini.

Hapa unaweza kuona Mtihani anaoupata Mtoto kama huyu wa darasa la kwanza tu ambaye hata kwa kumuangalia inaonesha kabisa kama hata amepata kifungua kinywa ni bahati....hivi kwa nini huyo Mwalimu asivae viatu vya huyu Mtoto?. Mwalimu anapata wapi msukumo wa kumshinikiza Mtoto alete hiyo mia tano kwa kumpiga yeye Mtoto anayepaswa kusubiri apewe pesa na Mzazi?.

Hapo huwa najiuliza Mwalimu anapoamua kumuadhibu Mtoto hivi ni kwamba hatumii akili kumbebesha Mtoto matatizo yasiyomuhusu? tena bila hata kujali hali ya huyo Mtoto mwenyewe.

Je kwa kauli hii ya Waziri itabadilisha nini ambacho hakijawahi kutamkwa kabla?.
kwanza mkuu Muumba akuongezee hapo ulipopunguza
jengine huko kwengine umeongea ukweli mtupu makosa ya wazazi wanapigwa watoto kweli dah!

Sent from my SM-J5108 using JamiiForums mobile app
 
Hahahahhaahaa wanasema ogopa sana kuongozwa politicians.Huyu waziri ni Mwanasheria kwa taaluma yake lakini hajui umuhimu wa mwanafunzi kuwa ndani ya sare ya shule inamwepusha na mambo mengi including masuala ya kiusalama kwake.Hivi akibakwa itakuwaje?
Viongozi wa TZ ni janga.
 
Tujitafakari haya mambo eti tupo uchumi wa kati. Ukweli usemwe uzazi wa mpango kuwapotosha watu elimu bure, huduma afya zimeboreshwa mfyatuane!!!
wewe kwa tafsiri yako uchumi wa kati ni upi?

Je tanzania imeji-rank yenyewe kuwa uchumi wa kati kwa kujipendelea?

Ikiwa zipo nchi nyingne ktk afrika hii kama Kenya, Ghana, Namibia Benin zipo pia uchumi wa kati, kwanini isiwe sisi!

Rankings za kisoka mnaziamini, za kiuchumi hamtaki!

Ungeambiwa hapo yanga au simba ni ya 7th ktk viwango vya ubora afrika usingesita kuamini.
 
"Kama Katiba ingeruhusu Mhe Samia Suluhu Hassan hakupashwa kuwa Rais wa mihula miwuli pekee,

Huyu Mama walau kwa Uchache angestahili miaka walau 15 "
kwasasa ndie waziri angalau anayeonekana kujiamini.

Labda na yule dogo wa pangani bwana awesso.
 
Bado michango inahimizwa na kupelekwa mashuleni kwa mgongo wa kinachoitwa "WAZAZI WAMEAFIKI"

Ni uhuni wa baadhi ya walimu..na ni wengi.

Kinachofanyika mwalimu mkuu anaitisha kikao na wazazi..

Wazazi wanaohudhuria wanakuwa ni wachache mno, probably chini ya 25%

Mwalimu mkuu ana-introduce mchango..
wazazi hao wanapitisha bila utaratibu wa kura..
mchango tayari..

mahudhurio yanachukuliwa na wakt mwingne idadi ya mahudhurio kughushiwa

Hapa serikali iondoe huu mkanganyiko..
ije na mwongozo kwamba michango ya aina yeyote shuleni; iwe ni ya hiari au ya mashaurino ipgwe marufuku..

Hizi ndimi mbili za serikali ndio wakt mwingne mzizi wa tatzo.
 
Team JF,


MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEAR 2022.

#TUENDELEE KUMUUNGA MKONO RAIS WETU,
 
Bado michango inahimizwa na kupelekwa mashuleni kwa mgongo wa kinachoitwa "WAZAZI WAMEAFIKI"

Ni uhuni wa baadhi ya walimu..na ni wengi.

Kinachofanyika mwalimu mkuu anaitisha kikao na wazazi..

Wazazi wanaohudhuria wanakuwa ni wachache mno, probably chini ya 25%

Mwalimu mkuu ana-introduce mchango..
wazazi hao wanapitisha bila utaratibu wa kura..
mchango tayari..

mahudhurio yanachukuliwa na wakt mwingne idadi ya mahudhurio kughushiwa

Hapa serikali iondoe huu mkanganyiko..
ije na mwongozo kwamba michango ya aina yeyote shuleni; iwe ni ya hiari au ya mashaurino ipgwe marufuku..

Hizi ndimi mbili za serikali ndio wakt mwingne mzizi wa tatzo.
UNAYO HOJA MKUU WANGU,
 
Mojawapo ya jambo linaloleta nidhamu mashuleni ya hali ya juu ni wanafunzi kulazimika kuvaa sale za shule zilizo nadhifu. Hili ni jambo ambalo linakubalika kwa wazazi/walezi na hata kwa uongozi wa shule husika.

Sasa kama mzazi amepewa unafuu wa kutokulipa ada, sasa huruma nyingine ya kijinga inaingia hata katika masuala muhimu ya kinidhamu. Hivi serikali inafikiria kuwa ili kumkomboa mtu maskini ni kwa kumsaidia kuishi kwake katika fikra za kifukara!?
Tujiondoe kwenye zama zile.
Hata hivyo amesema wapewe muda.
Nchi za wenzetu walioendelea hawana cha sare na wanasoma vizuri tu. Tubadilike.
 
Mambo ya ajabu sana kwa kuharibu utaratibu uliowekwa. Mwanafunzi lazima aende akiwa ndani ya uniform.

Kuwaruhusu kwenda bila uniform ni presence mbaya sana, siku tutawaruhusu waingie darasani hata kama hawana daftari.
Unform na Madaftari ni vitu viwili tofauti
 
===
Waziri wa TAMISEMI, Mhe Ummy Mwalimu amekemea utozaji wa michango mbalimbali kwa Wanafunzi Shuleni sanjari na vitendo vya baadhi ya Walimu kuwazuia Wanafunzi kuingia Shuleni kwa kukosa sare na mahitaji mengine yanayohitajika Shuleni hapo.

Amesema vitendo hivyo havikubaliki na kwamba Walimu hao wanapaswa kuwa na huruma kwa Wazazi na Walezi wa Watoto hao na kwamba wanapaswa kuhakikisha wanaepuka kuwakwamisha Watoto hao kusoma.

"Walimu wasiweke vikwazo kwa Watoto wanaoanza darasa la kwanza, Katibu Mkuu hakikisha unaandika waraka wa utaratibu, tunataka Shulr zinapofunguliwa January Watoto 90007 wa kidato cha kwanza waanze Shule"

Katika kulisisitiza hilo Waziri Ummy amesema anatafuta Shule mbili au tatu za kutolea mfano endapo zitabainika kutenda kosa hilo na kusisitiza kuwa Wazazi hawapaswi kubebeshwa mzigo kwa kuwa Serikali ilishaweka utaratibu wa elimu bila ada.

"Sitaki kuona Mwanafunzi amerudishwa kwasababu ya michango na kwa hawa wanaonza kidato cha kwanza hata kama hawana sare ya Shule aliyochaguliwa asirudishwe bali apewe muda”Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu akihutubia kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari za Serikali na Binafsi leo Dar es salaam


View attachment 2045856
Waziri Ummy chapa kazi Mama,
 
Back
Top Bottom