Waziri Ummy: Nakataza Michango Mashuleni, asiyekuwa na Sare za Shule acha asome

Nakumbuka form one headmaster alisema hatambui uniform nje ya shule lazima tutoe hela tupimishwe shuleni,tulitoa hela baadaye wanaume tumeletewa suruali nyeusi za mtumba
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Unadhani leo kwenye hizi shule hiyo maana ya uniform bado ni ile ile ya miaka hiyo?

Leo lengo kubwa ni pesa tu, mfano mzazi unaweza kupata uniform kwa gharama kidogo huku mtaani, lakini shule inataka ikuuzie yenyewe tena bei kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo uhuru wakianza kuutumia vizuri ndipo itafahamika kama wamesaidia au wameharibu.
Walau uniform zinasaidia hususan upande wa nidham wanapokuwa nje ya viunga vya shule.
Halafu juzi wamewaruhusu kupata mimba, za kuambiwa changanya na zako mbayuwayu....

1+1=
 
Logic nadhani ipo kwenye nembo ndio utapata shule.

Afadhali ya huko waulize diaspora wanaoishi UK wakwambie kwao huko nembo ya shule inawekwa kwenye masweta, halafu unakuta ni duka moja au mawili tu kwenye jimbo ndio yenye kibali cha kuuza.

Shule zikifunguliwa wanafunzi wapya wanaojiunga na hizo taasisi unakuta wazazi wamepanga mstari mrefu huo mbele ya duka karibu week nzima na bei yake ni masweta 3/4 hayo hayo dukani bila ya nembo.

Swala la uniform especially kwa Africa sio la mzaha, watoto wakifanya vurugu huko mtaani watu wanajua waende wapi.

Zama zetu kwenye adhabu ilikuwa bora utoroke ukamatwe ulivaa uniform. Lakini ukamatwe ujavaa uniform utajuta adhabu yake.

Uniform ni muhimu sana hasa kwa boarding schools.
 
Ni kwa form One tu mkuu
Tuna lea ujinga kesho watasema hawana madaftari, haya mambo ndiyo yanayo shusha hadhi ya elimu haya .
 
Uwelewa mbaya,ukiangalia shule za private mwanafunzi anafika shuleni Hana uniform anaenda darasani mpaka itakapokuwa tayari Sasa ubaya upo wapi wa wazazi kupewa muda huku mtoto akiendelea na masomo?
Tuache kufikiria negative kila kijacho
Kifupi tuna lea ujinga sare za shule zinasababu waache kingiza siasa kesho watasema hawana viatu na madaftari wazazi wanafunzwa uzembe
 
"Kama Katiba ingeruhusu Mhe Samia Suluhu Hassan hakupashwa kuwa Rais wa mihula miwuli pekee,

Huyu Mama walau kwa Uchache angestahili miaka walau 15 "
 
Sasa tutajuaje kama ni miaka 30 au ni hawa wa mtaani kina Mwajuma ndala ndefu?
 
Kaziiendelee dada Ummy,
 
Kaziiendelee
 
Sare ni nyenzo muhimu katika kutawala nidhamu ya watoto.

Pia kuhakikisha wanapata upendeleo unaostahili na kuepusha unyanyasaji dhidi yao.

Sare sio suala la kukurupuka. Ni nyenzo ya kisaikolojia inayotumika kwenye taasisi zote zenye kushughulika na idadi kubwa au hata ndogo ya watu ambapo nidhamu ya hali juu sana ni takwa muhimu.

Lakini pia ni utambulisho ambao unaweka wazi kwa jamii yote namna ya kushughulika na mhusika kama akipata tatizo au akiwa na mwenendo tofauti na unaotarajiwa na hali yake inayotambulishwa na sare alizovaa.

Sare kwa wanafunzi haina mbadala na wala haipaswi kuwa na exemption.
 
Kwani waziri wa Elimu anasemaje yeye?


Malimu anafundisha watoto wasio na UNIFORM. Huku anaonyesha, Huku ana Mimba. .HATAREE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…