JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Serikali imeanza mchakato wa ujenzi wa hospitali maalum ya magonjwa ya mlipuko na kituo kikuu cha uchunguzi mkoa wa Kagera kutokana na mkoa huo kupakana na nchi ambazo zimekuwa na historia ya kushambuliwa mara kwa mara na magonjwa hayo.
Akizungumza Mkoani Kagera wakati wa hafla ya uzinduzi wa kukabidhi vifaa vya kuwezesha wahudumu wa afya ya jamii kwa mikoa sita, Waziri wa Afya Mhe. Jenesta Mhagama amesema kuwa tayari ametembelea maeneo itakapojengwa hospitali na kituo hicho.
Ameongeza kuwa licha ya kuwa serikali tayari imeboresha huduma za afya katika vituo na hospitali mbalimbali bado kuna changamoto ya uwepo majengo ya mama na mtoto ambapo ameahidi kabla ya uchaguzi mkuu mwaka huu mpango wa kujenga jengo hilo katika hospitali ya Rufaa ya mkoa – Bukoba utakuwa umeanza.
Awali akimkaribisha Waziri wa Afya, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajat Fatma Mwassa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa pesa alizozitoa kwa sekta ya afya mkoani humo huku akimuomba Waziri kuletewa wataalamu wabobevu katika idala ya mionzi na usingi kwa kuwa vifaa tayari vipo.]
Baadhi ya wananchi wa mkoa huo wamesema kuwa uwepo wa hospitali hiyo itakuwa mwarobaini wa kukabiliana kwa haraka na kupunguza madhara ya magonjwa ya milipuko.
Aidha Waziri wa Afya amesema kuwa kupitia wahudumu wa afya ya jamii ambao wamekabidhiwa vifaa vya kuhudumia jamii watasaidia kuwa sehemu ya kubaini dalili za magonjwa ya milipuko kwa wakati.
Pia soma:
~ WHO: Watu nane wamefariki Kagera kwa ungojwa unahisiwa kuwa ni Marburg
~ Serikali yasema inafuatilia taarifa za uwepo wa Virusi vya Marburg Mkoani Kagera