Waziri wa afya Kenya apongezwa na magazeti ya Ulaya kwa jinsi anajituma na kuwa muwazi

Naamini kenya itachaguliwa kuwa sample ya dawa za korona kutestiwa kama zinafanya kazi na wazungu. Kazi kwenu kenya!
 
Wao ndio wameathirika sana huko ulaya, kwa nini waje testia dawa yao afrika ambako hakujaathirika sana kama wao? Kwa nini wasiende italy au spain?
 
Wanachosema Maprofesa hao ni chanjo ifanyiwe testing Africa sio itumike! ... Je Afrika ndo inaongoza kwa wagonjwa na vifo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hujatumia lugha yako ya asili au kiswahili kuwasilisha hoja yako? Waziri akipata 'recognition' ya kimataifa na kutajwa kama shujaa na media za kimataifa inahusiana vipi na rangi ya ngozi ya mtu yeyote yule? Health Cabinet Secretary Mutahi
Kagwe has earned international recognition after New York-based
publication Wall Street Journal recognised him as a hero in the fight against Covid-19.
Taarifa simple sana kama hii sio ya kumbabaisha mtu yeyote yule ambaye hana 'inferiority complex' na anajiaminia uafrika wake au rangi ya ngozi yake. Tena sio kwenye dunia ya sasa ambayo binadamu wote tupo 'interconnected'.
 
Wameanza kuonesha dhamira yao ... Imeanza siasa katika corona toka magharibi
Yamkini wanataka nasi afrika tuongeze kutangaza tuathirike kiuchumi zaidi ....
Wacha mola awe upande wetu kwa hili
 
Give credit where credit is due. Waziri anastahili sifa kwa jinsi anvyojituma.
Ndio nawashangaa hawa viumbe na hizi chorus zao za kawaida za mabeberu. Mtu anasifiwa kwa mafanikio yake binafsi tena na media moja tu kutoka NY alafu wao wanaanza kuingiza hadithi zao za kipumbavu. Naona ametajwa pamoja na wengine kutoka Korea na UK pia, sijui hawa wanakwaya watasema nini kuhusu hilo. Makali ya dozi la Ujamaa hadi sasa hivi bado hayajafifia.
 
Wao ndio wameathirika sana huko ulaya, kwa nini waje testia dawa yao afrika ambako hakujaathirika sana kama wao? Kwa nini wasiende italy au spain?
Yaani sijui Africa kwanini
Au kwavile hatujiwezi kwa hili wazungu wanatudharau sana... Wao ndo waloathirika zaidi lakini test AFRIKA
 
Wao ndio wameathirika sana huko ulaya, kwa nini waje testia dawa yao afrika ambako hakujaathirika sana kama wao? Kwa nini wasiende italy au spain?
Mbona walishaanza testing sehemu nyingi tu. Sasaqatajuaje kama dawa inawafaa wafrika kamnaingiza mambo ya rangi
 
Mbona walishaanza testing sehemu nyingi tu. Sasaqatajuaje kama dawa inawafaa wafrika kamnaingiza mambo ya rangi
Swali la msingi ni kwa nini testing afrika na sio italy ambako kuna sample nyingi za ugonjwa?
 
Yaani sijui Africa kwanini
Au kwavile hatujiwezi kwa hili wazungu wanatudharau sana... Wao ndo waloathirika zaidi lakini test AFRIKA
Kaka sisi waafrika tuna matatizo sana, sisi ni watu wa kulialia tu na kuhisi tunadharauliwa au kubaguliwa.
1) Katika chanjo zote tunazozitumia hapa Afrika, 90% majaribio yalifanyika kwa wazungu, lakini sisi ndio tunazitumia na kufaidika zaidi, sasa kuna tatizo gani hii chanjo majaribio yakifanyika Africa?.
2) Kabla ya kulalamika ni lazima ujue taratibu za "Clinical trials", na kwanini yule daktari wa ufaransa alipendekeza kuja kuifanyia majaribio hapa Africa.

Hebu tupunguze kulalamika kila Mara na kujiona dunia haitupendi bila kuwa na uwelewa mzuri katika haya mambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…