Naomba sana hiyo chanjo ije niwe wa kwanza kujaribisha ili kuokoa bara hili, mpaka leo Waafrika tumekoswa koswa na hiki kirusi, siku ukiskia kimetinga mitaa ya mabanda kama Tandale ndio ujue kiama cha Afrika kitakua kinaanza, wacha leo watu wanabweteka hovyoo. Mitaa ya mabanda hamuwezi kumudu lockdowns kama kule kwa wazungu, mtakufa njaa, hivyo tuombe mzungu agundue chanjo ya kutulinda mapema.
Wanasayansi wa Afrika wamekaa wanasubiri hadi mzungu avumbue dawa, hawachangii kwa chochote, leo profesa wa Ufaransa amejitokeza akisema chanjo ikipatikana itumike Afrika kwanza maana wote wanajua jinsi hali ilivyo huku, maeneo mengi hayana hata maji au huduma za msingi za kijamii uwaweke lockdown utawamaliza.
Waafrika bado sana, acheni kujifanya kichwa ngumu ilhali umaskini umetamalaki, jana tumeona Tanzania inawaomba msaada wa mkopo hao hao wazungu walioathirika, yaani ni kama uende kwa wenye msiba badala utoe mchango wa kuwasaidia, bila aibu unawapa kibakuli cha kuombea msaada.