Waziri wa Afya upi msimamo wa serikali? Wajawazito walipe au wasilipe? Kama wanalipa tupe orodha ya mahitaji na gharama

Waziri wa Afya upi msimamo wa serikali? Wajawazito walipe au wasilipe? Kama wanalipa tupe orodha ya mahitaji na gharama

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Waziri wa Afya nadhani umeona kauli ya RC. Naamini huo siyo msimamo wa CCm na serikali yake. Wewe kama Waziri mwenye dhamana unapaswa aidha kukemea au kuweka taarifa sawa la sivyo haya maelekezo ya RC yanakwenda kuwa msimamo wa watumishi wa afya kuanzia mjini hadi kijijini.

Kumbuka RC amesema kama huna pesa ya matibabu kaa kimya usijisumbue kwenda kwenye vyombo vya habari. Amekoleza kwamba kulalamika kwa kukosa pesa ni kufanya siasa.

Tunatambua wapo watu hata mlo mmoja kwao ni shida, hakuna mtu angependa kumwacha mpendwa wake afe na fedha anazo. Wenye fedha wapo private hospitals. Tupe msimamo wa serikali pls
 
Chalamila kaongea uhalisia wa maisha....

Endelea kukomaa na waziri (mwanasiasa), ambaye atakupa jibu la kisiasa, ila ukienda hospitali utalipia tu utake usitake..

Chalamila kawaambia "Punguzeni siasa"
 
Lugha aliyo tumia sio rafiki kabisa, hakumpasa kuongea vile japo ujumbe wake una hoja.
 
Lakini wakati ufike tuseme ukweli! Ngono na kungoneka ufanye wewe alafu kuzaa tugharimie wengine! Astaghafullulah! Wakati mimba imekaa miezi 9 hukujua utakuja kujifungua? Acha masikhara nyie waswahili!
 
Back
Top Bottom