#COVID19 Waziri wa Afya wa Uingereza augua Covid-19 baada ya kupata chanjo

Hayo wamekuachia na wewe usaidie kwasababu ndio mtu mwema sana.

Sasa wakifanya yote, wewe kazi yako dunia hii ni nini zaidi ya kupiga majungu mitandaoni.
 
Mwanzo tuliambiwa tunachanjwa tusipate Corona

Sasa hivi tunaambiwa tunachanjwa ili tukipata Corona tusiwe Mahututi

Kwny hili namkumbuka sana Mbabe JPM


Ona form ya chanjo.

Kwa nini serikali inajitoa?
 
Ni kama unabii wa Yeremia juu ya Israeli baada ya kumwasi Mungu, wakamuuliza sasa itakuwaje.......Yeremia akawajibu "Walioandikiwa kufa, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; au kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa, au kutekwa nyara, watakuwa mateka" soma Yeremia 15:2-3.
Lakini bado kulikuwa na masalia (survivors) ambao waliendelea kuishi......sasa hofu ya kifo au maangamizi kama hii covid-19 inatoka kwa ibilisi, lakini kuna watu wapo very desperate kujua ni lini chanjo zitafika ili waweze kupona, nani aliyewambia wapo kwenye kundi la kupona?

Lakini kuna wengine ambao hata hiyo hofu ya korona hawana, hawajali kama chanjo zitakuja au la, na unaweza kukuta miongoni mwao wapo ambao wapo kwenye kundi la kupona (survivors).

Kwa hiyo naungana na wewe kwamba hatima ya mwanadamu ipo kwa Mungu Mwenyezi, haya mengine ni kujazana hofu zisizo na msingi badala ya kuendelea kumtumainia Mungu pekee tunaendekeza hofu.
 
We Màtaga Acha ujinga,

Mfano chanjo ya Sulua ,siyo kwamba surua haipo,isipokuwa mtoto aliugua Sulua huwa Haina nguvu na mtoto au mgonjwa hupona kwa wepesi
 
Hayo wamekuachia na wewe usaidie kwasababu ndio mtu mwema sana.

Sasa wakifanya yote, wewe kazi yako dunia hii ni nini zaidi ya kupiga majungu mitandaoni.

We mzee wa siku nyingi huishiwi majungu..
Yego mkaruka
 
Mimi ninakwerwa na msamiati tu. Neno KUCHANJWA linanikera sana. Kwani hakuna kisawe chake?
 
Mama gwajima namuona vile mama anasema awe mfano kwa taifa tupate chanjo.
 
Mimi ninakwerwa na msamiati tu. Neno KUCHANJWA linanikera sana. Kwani hakuna kisawe chake?
Kuchoma sindano ya kinga,hili la kuchanjwa lao wao pale inayotumika Ni sindano Sio wembe Wala kisu,hivyo neno zuri Ni kuchoma sio kuchanjwa.
 
Ni kweli kabisa badala ya COVID-19 kukupeleka ulazwe hospitalini ukiwa mahututi na kuweza hata kuchungulia kaburi inakuwa ni ugonjwa wa kawaida tu. Sijui hii chanjo inakuwa na nguvu kwa muda gani.

Chanjo haizuii maambukizi ila inazuia hali kuwa mbaya baada ya maambukizi.
 
Ninaomba shule hapa. Baadhi mnasema kuwa katika kinga hii, mhusika anaweza kuambukizwa lakini kuugua kwake si kama yule asiye na kinga. Sasa nilitaka kujua, hii ni maalumu kwa covid pekee? Maana maradhi mengine ukishaambiwa umepata kinga basi unasahau. Kwa mfano, maradhi yale tunayokingwa utotoni. Tunasahau kabisa. Kwenye covid mbona lugha ni tofauti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…