Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,958
Waziri wa Afya wa Uingereza @sajidjavid amesema kuwa corona inaweza kuwepo milele hivyo inatubidi tuanze kuiona kama mafua na kujifunza kuishi nayo.
Aidha Javid amesema "inasikitisha lakini ni ukweli kuwa kuna miaka mingine huwa tunakumbwa na wimbi la mafua makali sana nayo huwa yanaua watu pia, ni lazima maisha yaendelee, muhimu ni kuangalia hali na kuchukua tahadhari stahiki, hatuwezi kuendelea kufunga nchi zetu sababu ya mafua.
“Ni muhimu tujipange kama tunavyofanya kwa mafua makali, watu huwa wanapewa nafasi ya kuchanjwa chanjo mara moja kwa mwaka haswa wazee.
“Huenda na chanjo ya Uviko19 ikawa hivyo, mara moja kwa mwaka, hatujui ila ndio mambo tunayotakiwa kuyafanyia kazi" amesema @sajidjavid
Itakumbukwa kuwa maneno haya aliwahi kuyasema mara Kwa mara hayati JPM kuhusu janga la Corona.
Kwasasa Dunia inaanza kuishi katika mawazo yake.